Sinopsis
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Episodios
-
Hofu ya raia zaidi kukimbia DRC kuelekea Burundi, UNHCR yasaka dola milioni 40.4 za kuwasaidia
21/02/2025 Duración: 02minShirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi, UNHCR limetoa ombi la dola milioni 40.4 ili kujiandaa na kutoa huduma za kuokoa maisha na usaidizi kwa wakimbizi wa ndani na waliokimbilia nchi jirani baada ya wakati huu ambapo mashambulizi ya waasi wa M23 yanazidi kufurusha raia kutoka Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokraia ya Congo, DRC. Anold Kayanda na maelezo zaidi.
-
Maelfu wavuka mto Rusizi kwa mtumbwi kutoka DRC na kuingia Burundi ili kuokoa maisha yao
21/02/2025 Duración: 05minMaelfu ya watu wanawasili nchini Burundi, wakikimbia mapigano yanayozidi kushamiri huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, hususan katika majimbo ya Kivu Kusini na Kivu Kaskazini. Waasi wa M23 wanaendelea kupanua wigo wa maeneo wanayomiliki, hali inayotumbukiza raia kwenye changamoto za usalama, na kulazimu wale wanaoweza kukimbia. Wengine wameuawa, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, na majeruhi wako hospitalini ambako huduma nazo zimedorora kwani M23 wamefunga barabara katika maeneo yote wanayodhibiti. Lakini wale wanaokimbilia Burundi hali yao iko vipi? Evarist Mapesa anakusimulia zaidi kupitia video iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR.
-
21 FEBRUARI 2025
21/02/2025 Duración: 11minHii leo jaridani tunaangazia mahitaji ya wakimbizi wanaokimbia machafuko DRC wakielekea nchini Burundi, na hali ya wakimbizi wa ndani Gaza wakati huu wa msimu wa baridi. Makala tunakurejesha nchini DRC na mashinani tunakwenda nchini Tanzania.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi, UNHCR limetoa ombi la dola milioni 40.4 ili kujiandaa na kutoa huduma za kuokoa maisha na usaidizi kwa wakimbizi wa ndani na waliokimbilia nchi jirani baada ya wakati huu ambapo mashambulizi ya waasi wa M23 yanazidi kufurusha raia kutoka Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokraia ya Congo, DRC.Huko Gaza Kaskazini, kwenye eneo la wapalestina linalokaliwa na Israeli, wanafamilia zilizofurushwa makwao kutokana na vita kati ya Israeli na wanamgambo wa Hamas wanavumilia msimu wa baridi kali katika makazi ya muda ya mahema yanayopigwa na upepo na mvua usiku na mchana, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF. Nyumba zao zimeharibika na kuacha watoto kuishi katika mazingira mabaya.Katika makala Evarist Map
-
Watoto watota kwa mvua katika ukanda Gaza, huku baridi kali ikitishia afya zao
21/02/2025 Duración: 02minHuko Gaza Kaskazini, kwenye eneo la wapalestina linalokaliwa na Israeli, wanafamilia zilizofurushwa makwao kutokana na vita kati ya Israeli na wanamgambo wa Hamas wanavumilia msimu wa baridi kali katika makazi ya muda ya mahema yanayopigwa na upepo na mvua usiku na mchana, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF. Nyumba zao zimeharibika na kuacha watoto kuishi katika mazingira mabaya. Ni sauti ya watoto wakitembea katikati ya mahema ya muda kwenye vichochoro vilivvyojubikwa na matope, hapa Gaza Kaskazini, huku wakijaribu kukwepa madimbwi ya maji yaliyosababishwa na mvua kubwa.Kupitia video iliyoandaliwa na UNICEF, Shahd Omar, msichana mwenye umri wa miaka kumi na saba, anaonekana amembeba nduguye, wengine wanaonekana wamekujikunyata kutokana na baridi. Shahd sasa akiwa amesimama nje hema lao anaelezea jinsi nyumba zao zilivyoharibiwa.“Tunavumilia hali ngumu sana,mvua kubwa, baridi, na upepo mkali, maisha ni magumu sana. Nyumba yetu ilivyoshambuliwa na kubomoka tulijitoa kwenye vif
-
Jifunze Kiswahili: Upatanisho wa kisarufi wa baadhi ya maneno
20/02/2025 Duración: 52sKatika kujifunza lugha ya Kiswahili Mlumbi wa Lugha Joramu Nkumbi kutoka Tanzania anafafanua upatanisho wa kisarufi wa baadhi ya maneno kama vile "Ng'ombe kumi na minane ", vikombe viwili na mengineyo ambayo watu hutamka vibaya katika sentensi, mfano "Ng'ombe kumi na nane"
-
20 FEBRUARI 2025
20/02/2025 Duración: 10minHii leo jaridani mada kwa kina ikimulika harakati za uhamasishaji kabla na baada ya maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani iliyoadhimishwa hivi karibuni na mchango wa redio katika juhudi za uhifadhi wa mazingira na kuchagiza maendeleo ya jamii huko Ramogi nchini DRC. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa maneno.Idadi ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC walioingia Burundi kufuatia mashambulizi yanayofanywa na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda, mashariki mwa DRC sasa imeongezeka na kufikia 20,000.Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP kupitia ukurasa wake wa X zamani Twitter, limechapicha picha zikionesha wakimbizi walio njiani wakipikiwa chakula, wakati huu ambapo M23 wametwaa miji ya Goma jimboni Kivu Kaskazini, na Bukavu na Kamanyola jimboni Kivu Kusini.Na katika hatua nyingine ofisi ya pamoja ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ikipatiwa jina UNJHRO imeripoti jinsi kutoroka kwa wafungw
-
Tanzania yataja mambo ya kuzingatiwa ili ulinzi wa amani uwe na tija
19/02/2025 Duración: 03minHistoria ya ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa ulianza miaka mitatu tu baada ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa wenyewe. Na kutokana na umuhimu wa ulinzi wa amani kote duniani, shughuli hiyo imedumu kwa miaka yote hiyo 77 hadi sasa na bado ni muhimu lakini inaendelea kukumbwa na changamoto kama anavyofafanua Brigedia George Mwita Itang’are wa Tanzania, moja ya nchi 10 duniani zinazochangia zaidi vikosi vya ulinzi wa amani.
-
OCHA yasihi kufunguliwa kwa viwanja vya ndege Goma na Kavumu - DRC
19/02/2025 Duración: 01minBaraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likifanya kikao cha dharura jijini New York, Marekani kujadili hali ya usalama inayozidi kuzorota kila uchao huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya kibinadamu nchini humo, Bruno Lermaquis amesema kupanuka kwa mzozo huo kumezidi kugharimu maisha na mustakabali wa raia. Selina Jerobon na maelezo zaidi.
-
19 FEBRUARI 2025
19/02/2025 Duración: 09minHii leo jaridani tunaangazia msaada wa kibinadamu nchini DRC, na simulizi y amkimbizi wa DRC aliyekimbilia nchini Uganda. Makala inatupeleka nchini Tanzania, namashinani nchini Kenya, kulikoni?Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likifanya kikao cha dharura jijini New York, Marekani kujadili hali ya usalama inayozidi kuzorota kila uchao huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya kibinadamu nchini humo, Bruno Lermaquis amesema kupanuka kwa mzozo huo kumezidi kugharimu maisha na mustakabali wa raia.Sina mpango tena wa kurejea nyumbani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ni kauli yake Twagirayesu Gato, mwanafunzi huyu raia wa DRC aliyekimbia nchini mwake mwaka jana na kuingia Uganda ambako sasa anapata hifadhi. Amesema hayo kwenye video ya shirika la Umoja wa MAtaifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR iliyochapishwa katika ukurasa wa YouTube wa shirika hilo.Makala inatupeleka nchini Tanzania ambako tunamsikiliza Brigedia Jenerali George Mwita Itang’ar
-
Mkimbizi kutoka DRC aliyekimbilia Uganda akumbuka ukatili uliofanywa na waasi
19/02/2025 Duración: 02minSina mpango tena wa kurejea nyumbani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ni kauli yake Twagirayesu Gato, mwanafunzi huyu raia wa DRC aliyekimbia nchini mwake mwaka jana na kuingia Uganda ambako sasa anapata hifadhi. Amesema hayo kwenye video ya shirika la Umoja wa MAtaifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR iliyochapishwa katika ukurasa wa YouTube wa shirika hilo. Kufahamu msingi wa kauli hiyo ya Twagirayesu, ungana na Sharon Jebiichi.
-
18 FEBRUARI 2025
18/02/2025 Duración: 10minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina leo inayotupeleka DRC katika mji wa Goma uliokuwa mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini ambao sasa uko mikoni mwa waasi wa kundi la M23. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ujumbe kutoka mashinani.Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, OHCHR imesema hali huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC inazorota kwa kasi kubwa, na kusababisha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, ukatili kama vile watu kuuawa kiholela, wakiwemo watoto, wakati huu ambapo waasi wa M23 yaripotiwa wametwaa mji wa Bukavu, jimboni Kivu Kusini.Wakati hayo ya kiendelea ndani ya DRC, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeripoti kuwa katika siku chache zilizopita, wakongo kati ya 10,000 na 15,000 wamevuka mpaka wa DRC na kuingia Burundi wakikimbia mapigano.Na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP limekaribisha mchango wa dola milioni 5 kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kusini. kwa ajili ya kujengea mnepo na kuimarisha upatika
-
Mradi wa ufugaji bora wa mbuzi umenikwamua – Mfugaji Kigoma
17/02/2025 Duración: 04minShirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO nchini Tanzania linaendelea kutekeleza Programu ya pamoja kwa mkoa wa Kigoma KJP iliyoanza kutekelezwa nchini humo mwaka 2017 na mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa lengo la kusaidia kutatua changamoto za kipekee za mkoa huo ikiwemo zitokanazo na kuhifadhi wakimbizi kutoka nchi jirani.Miongoni mwa miradi inayotekeleza ni ule wa kupatia wananchi mafunzo ya ufugaji bora wa mbuzi ili waweze kuinua kipato chao na vile kuimarisha lishe kwenye familia.Kupitia video ya FAO, utamsikia mnufaika wa mafunzo hayo kama anavyosimulia Assumpta Massoi kwenye makala hii.
-
Dola bilioni 6 zahitajika kusaidia kukabiliana na janga la kibinadamu nchini Sudan
17/02/2025 Duración: 01minKutokana na hali tete ya kibinadamu nchini Sudan, Umoja wa Mataifa na wadau wake leo Februari 17 jijini Genea, Uswisi, wamezindua mipango ya misaada ya kibinadamu na wakimbizi kwa mwaka huu 2025 kwa Sudan, wakihitaji jumla ya dola bilioni 6 kusaidia karibu watu milioni 26 ndani ya Sudan na kanda nzima. Selina Jerobon na maelezo zaidi.
-
17 FEBRUARI 2025
17/02/2025 Duración: 09minHii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu kwa wakimbizi na raia wa Sudan, na maradi wa lishe bora kwa watotot nchini Kenya. Makala inatupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Zambia, kulikoni?Kutokana na hali tete ya kibinadamu nchini Sudan, Umoja wa Mataifa na wadau wake leo Februari 17 jijini Genea, Uswisi, wamezindua mipango ya misaada ya kibinadamu na wakimbizi kwa mwaka huu 2025 kwa Sudan, wakihitaji jumla ya dola bilioni 6 kusaidia karibu watu milioni 26 ndani ya Sudan na kanda nzima.Mradi unaoendeshwa na serikali ya kenya na kupigwa jeki na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ambao ni wa kuboresha lishe kwa watoto kwa kugawa fedha taslim na elimu ya afya au NICHE (NISHI) umeleta nuru kwa wakazi wa Lokichar katika kaunti ya Turkana Kaskazini Mashariki mwa Kenya na miongoni mwa wanufaika ni Leah Akiru.Katika makala Assumpta Massoi kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO nchini Tanzania anakuletea mnufaika wa mafunzo ya ufugaji bora wa mbuz
-
Mradi wa NICHE umekuwa mkombozi wangu, asante UNICEF: Leah Akiru
17/02/2025 Duración: 02minMradi unaoendeshwa na serikali ya kenya na kupigwa jeki na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ambao ni wa kuboresha lishe kwa watoto kwa kugawa fedha taslim na elimu ya afya au NICHE (NISHI) umeleta nuru kwa wakazi wa Lokichar katika kaunti ya Turkana Kaskazini Mashariki mwa Kenya na miongoni mwa wanufaika ni Leah Akiru. Ungana na Flora Nducha kwa taarifa zaidi
-
Kenya tumepiga hatua kuhakikisha maendeleo ya ustawi wa jamii: Mary Wambui Munene
14/02/2025 Duración: 04minKikao cha 63 cha Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC kuhusu maendeleo ya ujamii kinakunja jamvi hii leo jijini New York Marekani baada ya majadiliano ya juma zima kuhusu maendeleo ya ustawi wa jamii, hatua zinazochukuliwa nan chi katika kufanikisha hilo na kuchagiza mshikamano wa kimataifa kutimiza lengo. Nchi mbalimbali zimetuma wakilishi kuanzia katika ngazi ya serikali, taasisi, mashirika yasiyo ya kiserikali na asasi za kiraia. Flora Nducha wa Idhaa hii amepata fursa kuzungumza na Mary Wambui Munene, mmoja wa washiriki kutokana Kenya. Ungana nao katika Makala hii
-
Mashambulizi yakishamiri DRC, sinfohamu yakumba wakimbizi
14/02/2025 Duración: 02minShirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, lina wasiwasi mkubwa kuhusu janga la kibinadamu linalozidi kuwa baya tena kwa kasi kubwa huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kwani kushindwa kufikia wahitaji kumekwamisha ufikishaji misaada ya harakati inahoyitajika. Anold Kayanda na ripoti kamili.
-
14 FEBRUARI 2025
14/02/2025 Duración: 11minHii leo jaridani tunaangazia machafuko na hali ya wakimbizi wa ndani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Makala inaturejesha hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na mashinani inatupeleka nchini Jamhuri ya Africa ya Kati (CAR), kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, lina wasiwasi mkubwa kuhusu janga la kibinadamu linalozidi kuwa baya tena kwa kasi kubwa huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kwani kushindwa kufikia wahitaji kumekwamisha ufikishaji misaada ya haraka inahoyitajika..Katika kitongoji cha Komanda jimboni Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, doria za pamoja zinazoendeshwa na walinda amani wanaohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO na jeshi la serikali FARDC zimeimarisha usalama kwenye maeneo ya raia.Makala leo inaturejesha hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kwenye mkutano wa 63 wa Baraza la Kiuchumi na Kijamii ECOSOC kuhusu maendeleo ya jamii. Flora Nducha amepata fursa ya kuzung
-
Doria za pamoja za MONUSCO na FARDC huko Ituri DRC zaimarisha usalama
14/02/2025 Duración: 01minKatika kitongoji cha Komanda jimboni Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, doria za pamoja zinazoendeshwa na walinda amani wanaohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO na jeshi la serikali FARDC zimeimarisha usalama kwenye maeneo ya raia. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.
-
Jifunze Kiswahili: maana za neno “MSUMBI”
13/02/2025 Duración: 57sKatika kujifunza lugha ya Kiswahili leo fursa ni yake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana za neno “MSUMBI”