Habari Za Un
30 JUNI 2025
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editor: Podcast
- Duración: 0:11:41
- Mas informaciones
Informações:
Sinopsis
Hii leo jaridani tunaangazia mkutano wa 4 wa ufadhili kwa ajili ya maendeleo FFD4 huko Sevilla Hispania, na siku ya Mabunge tukizungumza na mmoja wao kutoka Tanzania. Makala inatupeleka nchi Kenya na mashinani tunarejea huko huko Tanzania, kulikoni?Mkutano wa 4 wa ufadhili kwa ajili ya maendeleo FFD4 umeng’oa nanga rasmi leo huko Selilla Hispania kwa wito wa kuziba pengo la ufadhili wa maendeleo ili kutimiza ahadi ya kimataifa ya kutomwacha yeyote nyumba. Mkutano huo uliowaleta pamoja washiriki 2,500 kutoka nchi 150 wakiwemo wakuu wa nhi 50 na wadau wengine unasema kuna pengo la dola trilioni 4 katika ufadhili wa maendeleo linalohitaji kuzibwa.Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya mabunge ikijikita katika harakati za kuwezesha mabunge kufanikisha usawa wa kijinsia wakati huu ambapo Umoja wa Mataifa unaeleza ni kwa vipi Wanawake bado hawawakilishwi kwa kiwango cha kutosha katika mabunge ya kitaifa na ya mitaa duniani kote, jambo ambalo linapunguza haki zao za kisiasa na ushawishi wao juu ya sheria na bajeti..Katik