Habari Za Un

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 8:36:32
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Episodios

  • 25 JUNI 2025

    25/06/2025 Duración: 10min

    Hii leo Jarida linamulika ripoti ya nishati jadidifu duniani, Afrika ikiwa bado inasuasua; Harakati za mabaharia wanawake Somalia, Mpango wa Umoja wa Mataifa wa UN80 na baba na malezi ya mtoto nchini Tanzania.Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inayofuatilia maendeleo kuelekea kutimiza Lengo la Umoja wa Mataifa la Maendeleo Endelevu namba 7 (SDG 7) linaloangazia nafasi muhimu ya nishati mbadala imetoa wito wa ufadhili zaidi kwani ingawa asilimia 92 ya watu duniani sasa wanapata umeme, lakini watu milioni 666 wengi wao wakiwa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara bado hawapati umeme. Anold Kayanda na maelezo zaidi.Nchini Somalia, suala la usawa wa kijinsia katika sekta ya baharini limepatiwa kipaumbele kwenye mjadala kuhusu wanawake katika tasnia hiyo, mjadala uliofanyika kwenye mji mkuu Mogadishu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mabaharia inayoadhimishwa tarehe 25 mwezi Juni kila mwaka ikibeba maudhui Meli yangu isiyo na unyanyasaji. Sharon Jebichii anatupasha zaidi.Je wafahamu kuhusu UN80? Flo

  • 24 JUNI 2025

    24/06/2025 Duración: 09min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina nayomulika mabaharia wanawake, ambapo tunamsikia mmoja wao, Mary Jane Siy Chuan, Fundi wa Umeme melini,  akisema, “ninapoingia melini, wafanyakazi wengine wanahoji kama vile, kwa nini kuna mwanamke baharini.”Kukiwa na dalili za kuwa sitisho la mapigano kati ya Iran na Israel linaanza kushika mizizi, mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki, IAEA Rafael Grossi. ametoa wito kwa Iran kuanza tena ushirikiano na jumuiya ya kimataifa ili kupunguza mvutano unaoendelea kuhusu mpango wake wa nyuklia. Grossi amesema amempa Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, ombi la kukutana na kushirikiana, “akitilia mkazo kuwa hatua hii inaweza kufungua njia ya suluhisho la kidiplomasia kwa mgogoro wa muda mrefu” kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.Msemaji wa Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa (OHCHR) Thameen Al-Kheetan ameripoti leo kwamba hadi kufikia sasa takribani Wapalestina 410 wameuawa na jeshi la Israeli wakati wakijaribu kupata msaada kutoka kwa

  • TANLAP Tanzania tunahamasisha wanawake wengi kushiriki kwenye uchaguzi ili washiriki kuamua mambo yanayowahusu - Christina Kamili Ruhinda

    23/06/2025 Duración: 03min

    Katika mahojiano haya, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Mashirika yanayotoa huduma ya msaada wa kisheria nchini Tanzania, TANLAP, Christina Kamili Ruhinda alipozungumza na Anold Kayanda wa Idhaa hii kandoni mwa Mkutano wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW69 uliofanyika mapema mwaka huu hapa New York, Marekani, anaeleza wanavyotekeleza mpango wao wa kuhakikisha wanawake  wanapata nafasi zaidi kwenye meza za uamuzi nchini Tanzania.

  • Muziki waunganisha jamii zilizogawanyika Malakal nchini Sudan Kusini

    23/06/2025 Duración: 02min

    Katika juhudi za kuimarisha mshikamano na kurejesha matumaini miongoni mwa jamii zilizotengana kwa migogoro, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini, UNMISS, kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, hivi karibuni waliandaa tamasha maalum la muziki katika mji wa Malakal, jimbo la Upper Nile – eneo ambalo kwa miezi ya hivi karibuni limekuwa kitovu cha machafuko. Sharon Jebichii anatupasha zaidi

  • 23 JUNI 2025

    23/06/2025 Duración: 10min

    Hii leo jaridani tunaangazia mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran, na juhudi za kurejesha matumaini miongoni mwa jamii zilizotengana kwa migogoro Sudan Kusini.  Makala tunakwenda nchini Tanzania na mashinani nchini Kenya.Hali ya taharuki yaendelea kushuhudiwa Mashariki ya Kati kufuatia mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran mwishoni mwa wiki. Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki IAEA, Rafael Grossi, leo ametoa wito wa dharura wa shirika hilo kuruhusiwa kufika kwenye maeneo hayo yaliyoharibiwa, ili kutathmini kiwango halisi cha uharibifu.Katika juhudi za kuimarisha mshikamano na kurejesha matumaini miongoni mwa jamii zilizotengana kwa migogoro, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini, UNMISS, kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, hivi karibuni waliandaa tamasha maalum la muziki katika mji wa Malakal, jimbo la Upper Nile – eneo ambal

  • Baada ya Marekani kushambulia vito vya nyuklia vya Iran, IAEA yataka fursa kutathimini uharibifu

    23/06/2025 Duración: 01min

    Hali ya taharuki yaendelea kushuhudiwa Mashariki ya Kati kufuatia mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran mwishoni mwa wiki. Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki IAEA, Rafael Grossi, leo ametoa wito wa dharura wa shirika hilo kuruhusiwa kufika kwenye maeneo hayo yaliyoharibiwa, ili kutathmini kiwango halisi cha uharibifu. Flora Nducha na tarifa zaidi

  • Burundi yamwezesha mkimbizi fundi seremala kutoka DRC kuendeleza stadi yake na kujipatia kipato

    20/06/2025 Duración: 03min

    Burundi inaonesha kwa vitendo mshikamano na wakimbizi kwa kuwapa fursa ya kupata elimu, huduma za afya, ajira na huduma nyingine za kitaifa, na hivyo kuwasaidia kuchangia katika jamii wanamoishi. Miongoni mwa wakimbizi hao ni Amani Lukoo Elie kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC akiambana na mke wake na watoto 5 wamesaka hifadhi kusini-magharibi baada ya kukimbia mapigano jimboni Kivu Kaskazini. Kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, Assumpta Massoi amefuatilia kile wanachofanya sasa ili kuweza kujikimu.

  • UN: Mshikamano na wakimbizi uwe kwa vitendo na si maneno matupu

    20/06/2025 Duración: 01min

    Leo ni Siku ya Wakimbizi Duniani, mwaka huu ikibeba maudhui “Mshinamano na wakimbizi” na Umoja wa Mataifa umetaka mshikamano huo kwa vitendo wakati idadi ya watu wanaolazimika kufungasha virago na kukimbia makayo yao ikifikia kiwango cha kihistoria. Flora Nducha na taarifa zaidi

  • 20 JUNI 2025

    20/06/2025 Duración: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia siku ya Wakimbizi Duniani, mwaka huu ikibeba maudhui “Mshinamano na wakimbizi”, tukisikia ujumbe wa Umoja wa Mataifa na kazi wanazozifanya kuinua Maisha ya wakimbizi, na pia tunakuletea sauti za wakimbizi kutoka DRC, Burundi, Ethiopia na Sudan Kusini.Leo ni Siku ya Wakimbizi Duniani, mwaka huu ikibeba maudhui “Mshinamano na wakimbizi” na Umoja wa Mataifa umetaka mshikamano huo kwa vitendo wakati idadi ya watu wanaolazimika kufungasha virago na kukimbia makayo yao ikifikia kiwango cha kihistoria.Tukisalia na siku ya wakimbizi duniani tunaelekea  eneo la Mata, karibu na mpaka wa Ethiopia na Sudan Kusini, ambakomaelfu ya wakimbizi kutoka Sudan Kusini wanapokea msaada wa dharura kupitia juhudi za Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP. unaolenga kuwalinda baada ya kukimbia  mapigano makali nchini mwao. Nyibol Chueny Puok, mama wa watoto 4 ni miongoni mwao.Katika makala Assumpta Massoi kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia

  • Wakimbizi kutoka Sudan Kusini wanapatiwa msaada na WFP mpakani mwa Ethiopia

    20/06/2025 Duración: 02min

    Katika eneo la Mata, karibu na mpaka wa Ethiopia na Sudan Kusini, ambakomaelfu ya wakimbizi kutoka Sudan Kusini wanapokea msaada wa dharura kupitia juhudi za Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP. unaolenga kuwalinda baada ya kukimbia  mapigano makali nchini mwao. Nyibol Chueny Puok, mama wa watoto 4 ni miongoni mwao. Sharon Jebichi anatupasha zaidi...

  • Jifunze Kiswahili: Maana ya neno KIHORO

    19/06/2025 Duración: 40s

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "KIHORO!"

  • 19 JUNI 2025

    19/06/2025 Duración: 10min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina, ikiwa kesho tarehe 20 mwezi Juni ni siku ya kimataifa ya wakimbizi maudhui yakiwa Mshikamano na Wakimbizi, tunakupeleka kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma iliyoko kaunti ya Turkana, kaskazini-magharibi mwa Kenya.Uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje FDI umeshuka kwa mwaka wa pili mfululizo, ukihatarisha mustakabali wa maendeleo katika nchi zinazoendelea, kwa mujibu wa wa ripoti iliyotolewa leo na kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo UNCTAD. ikionya kuwa pengo la mitaji linaongezeka huku sekta muhimu kama nishati safi na miundombinu zikikosa ufadhili wa muda mrefu.Katika siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili wa kingono kwenye mizozo, Umoja wa Mataifa umetoa onyo kuwa ukatili wa kingono unazidi kutumika kama silaha ya vita huku wanawake na wasichana wakiathirika zaidi. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA "Huu si uharibifu wa bahati mbaya  ni uhalifu wa kivita. Na waathirika lazima wawe kiini cha aman

  • Guterres: Tuepushe kauli za chuki kwenye ujumbe chanya

    18/06/2025 Duración: 01min

    Leo Juni 18 ni siku ya kimataifa ya kupambana na kauli za chuki ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametumia ujumbe wake kwa siku hii kutoa onyo kuhusu hatari zinazoongezeka za chuki mtandaoni, hasa zikichochewa na akili mnemba au (AI) na  na majukwaa ya kidijitali. Flora Nducha na taarifa zaidi.

  • Ujumuishaji wazazi wa kiume kwenye malezi ya watoto waleta manufaa kwa jamii

    18/06/2025 Duración: 02min

    Katika Kaunti ya Kilifi, iliyoko pwani ya Kenya barani Afrika,  Mpango wa Kuboresha Lishe kwa kupatia jamii Fedha na Elimu ya Afya (NICHE) unasaidia kuwaelimisha wazazi kuhusu umuhimu wa baba na mama kulea watoto wao kwa pamoja, mradi unaotekelezwa na shirika la Umoja wa MAtaifa la kuhudumia watoto, UNICEF. Assumpta Massoi anamulika moja ya familia zilizonufaika.

  • 18 JUNI 2025

    18/06/2025 Duración: 10min

    Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Katibu Mkuu Guterres, wa siku ya kimataifa ya kupambana na kauli za chuki na mradi wa lishe bora kwa watoto huko Kilifi Kenya. Makala tunakwenda nchini Rwanda na mashinani nchini Ghana, kulikoni?Leo Juni 18 ni siku ya kimataifa ya kupambana na kauli za chuki ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametumia ujumbe wake kwa siku hii kutoa onyo kuhusu hatari zinazoongezeka za chuki mtandaoni, hasa zikichochewa na akili mnemba au (AI) na  na majukwaa ya kidijitali.Katika Kaunti ya Kilifi, iliyoko pwani ya Kenya barani Afrika, Mpango wa Kuboresha Lishe kwa kupatia jamii Fedha na Elimu ya Afya (NICHE) unasaidia kuwaelimisha wazazi kuhusu umuhimu wa baba na mama kulea watoto wao kwa pamoja, mradi unaotekelezwa na shirika la Umoja wa MAtaifa la kuhudumia watoto, UNICEF.Katika makala shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO, kwa kushirikiana na Serikali ya Rwanda, linaendelea kujenga uwezo wa kitaifa katika kuhimiza matumizi ya mbinu rafiki kwa ma

  • Mafanikio ya Mradi wa ACP MEAs 3 Rwanda katika kuboresha kilimo endelevu

    18/06/2025 Duración: 03min

    Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO, kwa kushirikiana na Serikali ya Rwanda, linaendelea kujenga uwezo wa kitaifa katika kuhimiza matumizi ya mbinu rafiki kwa mazingira katika kilimo pamoja na usimamizi salama wa viuatilifu. Hili linafanyika kupitia utekelezaji wa awamu ya tatu ya mradi wa ACP MEAs 3 unaofadhiliwa na Muungano wa Ulaya EU. Mpango huu unalenga kuwawezesha wakulima wadogo kuhamia kwenye mifumo ya kilimo endelevu kimazingira na kuwajengea uwezo wa utekelezaji wa mikataba ya kimataifa ya mazingira. Sharon Jebichii anatupeleka nchini humo kumulika mradi huo..

  • Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetunga sera jumuishi zinazotetea haki za watu wenye ulemavu - Abeida Rashid Abdallah

    17/06/2025 Duración: 06min

    Mahojiano hayo leo inamulika juhuddi za Serikali ya Mapinzudi ya Zanzibar katika kuwajumuisha watu wenye ulemavu kwenye masuala mbalimbali katika jamii, Abeida Rashid Abdallah Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto ya kisiwani humo hivi karibununi akiwa kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kushiriki mkutano wa 69 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW69 alizungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii ungana nao

  • 17 JUNI 2025

    17/06/2025 Duración: 09min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika juhuddi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuwajumuisha watu wenye ulemavu kwenye masuala mbalimbali katika jamii, tukipata ujumbe wa Abeida Rashid Abdallah Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto ya kisiwani humo amabye hivi karibuni alihudhuria mkutano wa CSW69.Watu wa Ukraine hawapaswi kulazimika kujificha kusaka hifadhi kila jua lizamapo, amesema Matthias Schmale, Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa Misaada ya Kibinadamu nchini humo, kufuatia mashambulizi ya usiku wa kuamkia leo yaliyofanywa na jeshi la Urusi huko Kyiv, Odesa na miji mingine na kuua raia 12 na kujeruhi wengine zaidi ya 50.Mfumo wa afya wa huko Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli unazidi kudarimika, ukizidiwa uwezo kutokana na idadi kubwa ya watu waliouawa au kujeruhiwa karibu na maeneo ya usambazaji wa misaada, amesema Afisa wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya, WHO Dkt. Thanon Gargavanis. Akizungumza na waandishi wa habari Geneva, U

  • Akili mnemba na watu wenye ulemavu ni moja ya ajenda za COSP18 tutakazozingatia Tazania: Mpanju

    16/06/2025 Duración: 02min

    Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa 18 COSP18 wa mkataba wa watu wenye ulemavu CRPD, uliokunja jamvi mwishoni mwa wiki kwenye Makao Mkuu ya Umoja wa Mataifa ulijadili ajenda mbalimbali za kuhakikisha watu wenye ulemavu wanajumuisha, kushirikishwa na kutoachwa nyumba. Amon Anastaz Mpanju Naibu Katibu Mkuu wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum nchini Tanzania alikuwa miongoni mwa washiriki wa mkutano huo na aliketi chini na kuzungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii ambaye alitaka kufahamu  ni nini kikubwa anachoondoka nacho kwenye mkutano huo kitakachofanyiwa kazi Tanzania na kuleta tija kwa watu wenye ulemavu.

  • FAO/WFP: Nchi 13 katika ongezeko la njaa, 5 kati ya hizo wanakabiliwa na njaa kali zaidi

    16/06/2025 Duración: 01min

    Ripoti mpya ya pamoja ya Umoja wa Mataifa inaonya kuwa watu katika nchi 5 kati ya nchi 13 zenye njaa kali duniani wako kwenye hatari kubwa ya kukumbwa na njaa kali, vifo na maafa ikiwa msaada wa kibinadamu hautatolewa haraka na juhudi za kimataifa hazitaelekezwa kukomesha migogoro, kupunguza ufurushwaji na kuongeza msaada wa haraka kwa kiwango kikubwa. Anold Kayanda na taarifa zaidi.

página 2 de 5