Sinopsis
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Episodios
-
Tofauti ya maana ya maneno Ajali na Ajari, hasa pale yatakapotamkwa kwa kuchanganya herufi ‘R’ na ‘L’
17/10/2024 Duración: 01minKatika kujifunza lugha ya kiswahili, matamshi sahihi ya lugha husaidia kufikisha ujumbe sahihi. Kinyume cha hivyo ujumbe utakuwa sivyo ndivyo na ndio maana hii leo, mbobezi wa lugha ya Kiswahili, Joramu Nkumbi kutoka Tanzania anafafanua tofauti ya maana ya maneno Ajali na Ajari, hasa pale yatakapotamkwa na mzungumzaji anayechanganya herufi ‘R’ na ‘L’
-
17 OKTOBA 2024
17/10/2024 Duración: 11minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kufuatilia juhudi za vijana hasa katika kuboresha mifumo ya elimu katika matumizi ya teknolojia ambapo Gloria Anderson, Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Shirika la TEDI anatufafanulia zaidi.Leo ni siku ya kimataifa ya kutokomeza umaskini duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema umaskini umesalia kuwa baa la dunia ukiathiri mamia ya mamilioni ya watu duniani kote.Huko MAshariki ya Kati, awamu ya pili ya utoaji wa chanjo dhidi ya polio imekamilika eneo la kati mwa Gaza, ambapo Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus amesema watoto 181,429 wamepatiwa. Wengine 148,064 wamepatiwa matone ya vitamini A. Ingawa hivyo vituo vinane vya afya vitasalia wazi ili kuendelea kutoa chanjo kwa familia zilishindwa kufikisha watoto wao katika siku tatu za chanjoMkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika, Dkt. Matshidiso Moeti amezuri Rwanda kujionea harakati za taifa hilo k
-
Asante WFP sasa najua kuandika na kusoma jina langu – Mkimbizi DRC
16/10/2024 Duración: 03minMbali na usaidizi mkubwa kwa watu waliokimbia makazi yao kutokana na migogoro mashariki mwa DRC, shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) linatoa msaada kupitia miradi iliyo ndani ya mfumo wa kuzuia na kupunguza hatari za unyanyasaji wa kijinsia unaohusishwa na uhakika wa kupata chakula. Takriban wanawake 40 waliokimbia makazi yao wanaoishi katika kambi ya Bulengo jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa DRC wamenufaika na mafunzo ya kusoma na kuandika tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2024. Walengwa waliojifunza kusoma na kuandika wanashuhudia kwamba yamebadilisha maisha yao. Mwandishi wetu wa habari mashariki mwa DRC, George Musubao alisafiri kutoka Beni hadi Goma katika kambi ya Bulengo kuzungumza na mmoja wao.
-
Kambi ya huduma za macho ya UNICEF yawezesha watoto kuona vema
16/10/2024 Duración: 02minNchini Kenya, Idara ya Taifa ya Ulinzi wa Jamii kwa kushirikiana na Baraza la Kitaifa la watu wenye ulemavu na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF, wameendesha kambi ya kusaidia uoni kwa watu wenye changamoto. Mmoja wa wanufaika wa juhudi hii ni Candy, msichan wa mwenye umri wa miaka 7 ambaye ana ualbino.Akiwa mwingi wa matumaini, Eric Odhiambo Okeyo, baba mzazi wa mtotohuyo alimpeleka kwenye kambi hiyo jijini Kisumu ambapo alifanyiwa uchunguzi na matibabu.Baada ya kufanyiwa uchunguzi, Candy alielekezwa kwa daktari wa macho ili abaini aina ya miwani ambayo ingemfaa.“Mtoto alipoanza shule niligundua kwamba mwendo wake katika masomo ulikuwa wa polepole sana na pia alikuwa analamika kwamba haoni anachoandika mwalimu. Hata akienda kucheza niliona kwamba alikuwa akifunga macho mara kadhaa. Ilikuwa inanikosesha amani kwa sababu nilihisi kuwa alikuwa akiteseka,” amesema Eric.Mpango huu wa kielelezo wa UNICEF na wadau wake unashughulikia c
-
16 OKTOBA 2024
16/10/2024 Duración: 09minHii leo jaridani tunaangazi siku ya chakula duniani ikitupeleka jijini Roma Italia kufuatilia maadhimisho yake. Pia tunakupeleka nchini Kenya kusikia ni kwa jinsi gani mashirika wanhaha kusaidia uoni kwa watu wenye changamoto. Makala tunakwengda nchini DRC na mashinani Sierra Leone, kulikoni?Washiriki wa Sherehe za kimataifa za mwaka huu wa 2024 za kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Chakula zilizofanyika leo katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) jijini Roma Italia wamesisitiza haja ya upatikanaji wa vyakula mbalimbali vya kutosha, vyenye lishe, bei nafuu na salama.Nchini Kenya, Idara ya Taifa ya Ulinzi wa Jamii kwa kushirikiana na Baraza la Kitaifa la Watu wenye ulemavu na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, wameendesha kambi ya kusaidia uoni kwa watu wenye changamoto ikiwemo Candy mwenye umri wa miaka 7 ambaye ana ualbino. Baba yake alifika kwenye kambi hiyo na anatusimulia kupitia video ya UNICEF Kenya.Makala inatupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
-
Maadhimisho ya kimataifa ya siku ya chakula duniani yaangazia haki ya chakula salama chenye lishe na cha bei nafuu
16/10/2024 Duración: 01minWashiriki wa Sherehe za kimataifa za mwaka huu wa 2024 za kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Chakula zilizofanyika leo katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) jijini Roma Italia wamesisitiza haja ya upatikanaji wa vyakula mbalimbali vya kutosha, vyenye lishe, bei nafuu na salama.Ni maadhimisho ambayo yamewaleta wadau wa kilimo na chakula kutoka kote duniani lakini yanakuja huku kukiwa na mvutano na mizozo ya kimataifa na majanga ya tabianchi ambayo ni miongoni mwa mambo yanayochangia changamoto ya mamia ya mamilioni ya watu duniani kote kukabiliwa na njaa na mabilioni ya watu kushindwa kumudu chakula bora, FAO inaeleza katika taarifa iliyochapishwa katika ukurasa wake wa wavuti.Katika hotuba yake ya ufunguzi Mkurugenzi Mkuu wa FAO, QU Dongyu, amesema mifumo ya kilimo cha chakula inabidi "kusaidia wakulima wadogo, wakulima wa ngazi ya familia na wafanyabiashara wadogo katika mnyororo wa thamani ambao katika nchi nyingi ni wa msingi katika kufanya vyakula vyenye lishe, v
-
15 OKTOBA 2024
15/10/2024 Duración: 10minHii leo jaridani kesho ikiwa ni siku ya chakula duniani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kufuatili juhudi za FAO za kuhakikisha haki ya chakula kwa maisha bora na mustakabali bora kwa wananchi. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani.Licha ya mashambulizi, awamu ya pili ya chanjo kwa watoto dhidi ya polio huko Gaza iliyoanza jana imeendelea leo Jumanne eneo la kati mwa Gaza na hadi sasa watoto wapatao Elfu 93 wenye umri wa chini ya miaka 10 wameshapatiwa dozi ya pili.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP hii leo linatoa wito wa msaada wa dharura kuepusha janga la kibinamu eneo la kusini mwa Afrika kutokana na ukame uliochochewa na El- Niño.Na ubia mpya wa kutokomeza watu kukosa utaifa umezinduliwa huko Geneva, Uswisi ukilenga kutokomeza hadhi hiyo inayoathiri mamilioni ya watu duniani. Zaidi ya nchi 100, mashirika ya kiraia, taasisi zinazopigia chepuo kuondokana na hadhi hiyo, wanazuoni na wadau wengine wameanzisha ubia huo ikiwa ni kuendeleza kampe
-
Wagonjwa majeruhi wa vita 16 wahamishwa kutoka hospitali ya Kamal Adwan kuwapeleka katika hospitali ya Al-Shifa
14/10/2024 Duración: 03minOperesheni ya vikosi vya jeshi la Israel inayoendeea Kaskazini mwa Gaza kwa njia ya anga na ardhini kukabiliana na wapiganaji wa kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas yamelifanya eneo hilo kukatwa na sehemu zingine za Gaza, kwa kiasi kikubwa raia wakikosa huduma za msingi kama chakula, elimu na matibabu. Hospitali karibu zote Gaza Kaskazini hazifanyi kazi na iliyosalia ni Kamal Adwan nayo ikitoa huduma kwa kiasi kidogo sana kutokana na ukosefu wa vifaa, wahudumu wa afya na mafuta. Majeruhi wa vita wamezidi uwezo wa hospitali hiyo ndio maana ikaamua kuomba msaada kutoka shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO kuhamisha majeruhi hao kwenda hospitali Al-Shifa mjini Gaza. Katika makala hii Flora Nducha anamulika zoezi hilo la kuhamisha majeruhi.
-
UNICEF yatoa mafunzo ya kutengeneza sodo kwa kijana mkimbizi wa dani nchini Sudan
14/10/2024 Duración: 02minSodo au taulo za kike, vile vile pedi, ni muhimu kwa wanawake na wasichana, lakini wengi hawawezi kuzipata wakati wa vita na ukimbizi. Leo tunakutana na Samer, mvulana huyu ambaye akiwa na umri wa miaka 16 tu, kwa msaada wa klabu ya usafi ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF, anatengeneza na kusambaza sodo kwa wanawake na wasichana katika maeneo ya wakimbizi wa ndani jimboni Atbara, nchini Sudan. Msaada wa kifedha kutoka Mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa CERF, vilabu vya usafi vya UNICEF, na Shirika la Marekani la misaada ya maendeleo USAID, vijana wakimbizi wa ndani wanawezeshwa kupata suluhisho kwa changamoto za usafi wanazokutana nazo, wakati wa vita na ukimbizi. Mmoja wa vijana hawa wakimbizi ni Samer mvulana mwenye umri wa miaka 16, ambaye amefundishwa kutengeneza sodo na sasa, anazisambaza bure kwa wanawake na wasichana wakimbizi wa ndani katika jimbo la Atbara, nchini Sudan.Nikataka kujua jinsi Samer anatengeneza sodo hizo…"Nashona kati ya vipa
-
14 OKTOBA 2024
14/10/2024 Duración: 10minHii leo jaridani tunaangazia masuala ya afya katika ukanda wa Gaza yakiwa ni pamoja na chanjo dhidi ya polio huku mashambulizi ya Israel yakiendelea, na kuwahamisha wagonjwa majeruhi. Pia tunaangazia mchango wa wakimbizi Sudan kwa jamii, na ndoa za utotoni Zambia.Mashambulizi yakiendelea kurindima kutoka pande hasimu, jeshi la Israeli na wanamgambo wa Hamas huko Gaza, na Hezbollah huko kusini mwa Lebanon, mashirika ya Umoja wa Mataifa yameendelea na awamu ya pili ya chanjo dhidi ya Polio Ukanda wa Gaza, huku huko Lebanon ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura ikisihi raia wasilengwe.Sodo au taulo za kike, vile vile pedi, ni muhimu kwa wanawake na wasichana, lakini wengi hawawezi kuzipata wakati wa vita na ukimbizi. Leo tunakutana na Samer, mvulana huyu ambaye akiwa na umri wa miaka 16 tu, kwa msaada wa klabu ya usafi ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF, anatengeneza na kusambaza sodo kwa wanawake na wasichana katika maeneo ya wakimbizi wa ndani
-
Awamu ya 2 ya chanjo dhidi ya Polio Gaza yaanza licha mashambulizi
14/10/2024 Duración: 03minMashambulizi yakiendelea kurindima kutoka pande hasimu, jeshi la Israeli na wanamgambo wa Hamas huko Gaza, na Hezbollah huko kusini mwa Lebanon, mashirika ya Umoja wa Mataifa yameendelea na awamu ya pili ya chanjo dhidi ya Polio Ukanda wa Gaza, huku huko Lebanon ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura ikisihi raia wasilengwe. Naanzia eneo la kati mwa ukanda wa Gaza ambako asubuhi ya leo Jumatatu awamu ya pili ya chanjo dhidi ya polio imeanza ikilenga watoto 591 700 wenye umri wa chini ya miaka 10, watakaopatiwa dozi ya pili ya chanjo hiyo kufuatia kuthibitishwa kwa polio Gaza mwezi Agosti mwaka huu.Chanjo inatolewa licha ya ripoti za makombora kurushwa kwenye shule moja iliyogeuzwa makazi ya wakimbizi huko Nuseirat na katika hospitali moja huko Deir Al-Balah ambako mahema kadhaa yaliteketezwa kwa moto wakati watu wamelala.Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA, Louise Wateridge akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa amesema,&n
-
FAO yaleta nuru kwa wafugaji walioathiriwa na vita Gaza
11/10/2024 Duración: 03minMwaka mmoja wa vita katika ukanda wa Gaza iliyochochewa na mashambulizi ya Hamas dhidi ya Israeli Oktoba 7, 2023 na kisha Israeli kujibu mashambulizi yanayoendelea hadi leo, umekuwa ukimulika zaidi madhara ya vifo na majeruhi. Lakini sasa shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO limekusogezea madhara ya vita katika kilimo na ufugaji na ndio makala yetu ya leo ikisimuliwa na Assumpta Massoi.
-
Guterres: Ni wakati muafaka sisi kuwasikiliza wasichana
11/10/2024 Duración: 01minIkiwa le oni Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito wa kuwapa sikio watoto wa kike akianza ujumbe wake mahususi kwa ajili ya siku hii akisema uwezo wa wasichana zaidi ya bilioni 1.1 duniani hauna kikomo lakini tunapokaribia tarehe mwaka 2030, wa mwisho kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu, ulimwengu unaendelea kuwaangusha wasichana.“Wasichana wanachangia zaidi ya asilimia 70 ya maambukizi mapya ya Virusi Vya Ukimwi, VVU” anasema Guterres na kwamba wana uwezekano mara mbili zaidi wa wavulana kukosa elimu au mafunzo. Na ndoa za utotoni bado zimeenea, huku takriban msichana mmoja kati ya watano duniani akiolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18. Kotekote duniani, mafanikio yaliyopatikana kwa bidii ya usawa wa kijinsia yanafutwa na vita dhidi ya haki za kimsingi za wanawake na wasichana, na kuhatarisha maisha yao. kuzuia uchaguzi wao, na kuweka kikwazo cha mustakabali wa wasichana.Kwa kutumia kaulimbiu ya mwaka huu ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike ambayo
-
11 OKTOBA 2024
11/10/2024 Duración: 09minHii leo jaridani tunaangazia siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike na juhudi za Umoja wa Mataifa za kutokomeza ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na unaofanyika mtandaoni. Makala tunakupeleka katika ukanda wa Gaza, na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito wa kuwapa sikio watoto wa kike akisema uwezo wa wasichana zaidi ya bilioni 1.1 duniani hauna kikomo lakini tunapokaribia mwaka 2030, wa mwisho kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu, ulimwengu unaendelea kuwaangusha wasichana.Nchini Ethiopia hususan katika jimbo la Somali, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limechukua hatua kusaidia manusura wa ukatili wa kijinsia kuweza kujenga upya maisha yao wakati huu ambapo takwimu za shirika hilo zinaonesha kuwa zaidi ya wanawake na wasichana milioni 370 duniani kote wamekumbwa na ukatili wa kingono wakati wa utoto wao, yaani kabla ya kutimiza umri wa miaka 15.Makala tunakupeleka Gaza ambapo mwaka m
-
UNICEF nchini Ethiopia yarejesha matumaini kwa manusura wa ukatili wa kingono
11/10/2024 Duración: 01minNchini Ethiopia hususan katika jimbo la Somali, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limechukua hatua kusaidia manusura wa ukatili wa kijinsia kuweza kujenga upya maisha yao wakati huu ambapo takwimu za shirika hilo zinaonesha kuwa zaidi ya wanawake na wasichana milioni 370 duniani kote wamekumbwa na ukatili wa kingono wakati wa utoto wao, yaani kabla ya kutimiza umri wa miaka 15. Sauti hiyo ya Nasteyo Sahane Layle, Meneja wa kushughulikia visa vya ukatili wa kijinsia dhidi ya akina mama, watoto na wanawake hapa Gode, jimboni Somali mashariki mwa Ethiopia akisema kuwa kazi kubwa tunayoifanya ni visa vinavyohusu ukatili wa kingono.Ni katika video ya UNICEF iliyochapishwa kuonesha kiza kinachokumba watoto wa kike hususan leo ambayo ni siku ya kimataifa ya mtoto wa kike.Hapa Gode, UNICEF imeanzisha kituo hicho cha kutoa huduma zote na sasa kimekuwa ni kama eneo salama kwa manusura wa ukatili wa kingono.Anaonekana mmoja wa wasaka huduma kituoni hapa akifika tayari kupatiwa huduma, su
-
Jifunze Kiswahili: Ufafanuzi wa methali “Mapenzi ni kikohozi hayawezi kufichika.”
10/10/2024 Duración: 01minKatika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu hii leo ni Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “Mapenzi ni kikohozi hayawezi kufichika.”
-
10 OKTOBA 2024
10/10/2024 Duración: 11minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika malengo ya maendeleo endelevu. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwema za Lebanon, afya ya akili na ripoti ya UNICEF kuhusu ukatili wa kingono. Katika kujifunza Kiswahili tunakuletea uchambuzi wa methali.Nchini Lebanon ujumbe wa jeshi la Umoja wa Mataifa la mpito nchini humo, UNIFIL, unasema mapigano kati ya jeshi la Israeli, IDF, na wanamgambo wa Hezbollah kusini mwa Lebanon yamekuwa na madhara kwa ujumbe huo kwani makao yake makuu huko Naqourra na maeneo ya karibu yameshambuliwa mara kwa mara tangu kuanza kwa mapigano kati ya pande hizo mbili.Leo ni siku ya afya ya akili duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake amesisitiza udharura wa kupatia kipaumbele afya ya akili pahala pa kazi.Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linasema zaidi ya wasichana na wanawake milioni 370 walioko hai hii leo, walikumbwa na ukatili wa kingono wakati wa utoto wao, yaani kabla ya
-
Utoaji wa chanjo dhidi ya mpox nchini DRC
10/10/2024 Duración: 03minJamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imeanza chanjo dhidi ya ugonjwa wa homa ya Nyani au MPOX mwishoni mwa wiki iliyopita. Hii ni hatua muhimu ya kuongeza juhudi zinazoendelea za kupambana na mlipuko wa ugonjwa huo ambao DRC inachangia asilimia 90 ya wagonjwa wote zaidi ya 18,000 duniani. Lengo sasa ni kuokoa maisha, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO, kanda ya Afrika. Shuhuda wetu wakati wa kuanza kazi ya kutoa chanjo alikuwa mwandishi wetu wa Mashariki mwa DRC, George Musubao kutoka Goma, jimboni Kivu Kaskazini.
-
09 OKTOBA 2024
09/10/2024 Duración: 09minHii leo jaridani ikiwa ni siku ya posta duniani tunaangazia huduma za posta na juhudi za mashirika za kukabiliana na Mpox nchini DRC. Makala tunasalia huko huko DRC kufuatilia uzinduzi wa chanjo dhidi ya ugonjwa huo huo, na mashinani tunakupeleka nchini Lebanon.Leo siku ya posta duniani huduma ambayo ilionekana kuwa itasambaratika kufuatia ujio wa maendeleo ya teknolojia ya intaneti lakini wenyewe wasimamizi wa huduma hii duniani wanasema licha ya mtikisiko sasa mambo yanashamiri, siri kubwa ikiwa ni ubia badala ya ushindani.Ukisikia makovu yasiyofutika ni ya simulizi hii utakayoisikia kuhusu familia moja huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kupoteza watoto wanne kutokana na ugonjwa wa homa ya nyani au mpox huku mustakabali wao ukisalia mashakani kwani bado hawafahamu hali itakuwa vipi kwenye familia yao, baba na mama wakipambana na ugonjwa huo.Makala inatupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambapo chanjo dhidi ya mpox imeanza.Na mashinani tutaelekea Lebabon ambapo, tutasikia simu
-
Shirika la Umoja wa Mataifa la Posta lahimili changamoto kwa kugeuza changamoto kuwa fursa
09/10/2024 Duración: 02minLeo siku ya posta duniani huduma ambayo ilionekana kuwa itasambaratika kufuatia ujio wa maendeleo ya teknolojia ya intaneti lakini wenyewe wasimamizi wa huduma hii duniani wanasema licha ya mtikisiko sasa mambo yanashamiri, siri kubwa ikiwa ni ubia badala ya ushindani. Tunasherehekea miaka 150 ya shirika la Umoja wa Mataifa la Posta, UPU, tunatambua umuhimu wa moja ya mifano ya mapema zaidi ya ushirikiano wa kimataifa. Ni Masahiko Metoki, Mkurugenzi Mkuu wa UPU katika ujumbe wake wa siku hii adhimu akiongeza kuwa..“Kile kilichoanza na wanachama 22 sasa inajumuisha nchi 192, kikionesha uthabiti wa ushirikiano wa kimataifa.”Miaka 150 wamekumbana na changamoto, vita, majanga mabadiliko ya kasi ya teknolojia ya kidijitali. Lakini wanafanya nini?“Leo hii UPU inaongoza juhudi za kufanya huduma za posta kuwa za kisasa na bora. Inatoa fursa kwa nchi kushirikishana ufahamu, kusaka majawabu na kukabili changamoto za sasa. Moyo wetu wa ushirikiano ndio umetusaidia kugeuza vikwazo kuwa fursa na kufany