Habari Za Un

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 8:36:32
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Episodios

  • 16 JUNI 2025

    16/06/2025 Duración: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia baa la njaa katika nchi 13 duniania amabzo hakuna uhakika wa chakula, na hali ya kibinadamu kwa wakimbizi wa DRC. Makala tunasalia hapa makao makuu na mashinani tunakwenda nchini Nepal, kulikoni?Ripoti mpya ya pamoja ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo jijini Roma, Italia inatahadharisha kuwa watu katika nchi 5 kati ya nchi 13 zenye njaa duniani wako kwenye hatari kubwa ya kukumbwa na njaa kali, vifo na maafa ikiwa msaada wa kibinadamu hautatolewa haraka na juhudi za kimataifa hazitaelekezwa kukomesha migogoro, kupunguza ufurushwaji na kuongeza msaada wa haraka kwa kiwango kikubwa.Huko jimboni Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, juhudi za kidiplomasia zinaendelea kumaliza mapigano, huko nalo shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP likitoa wito wa msaada kwa watu waliofurushwa makwao kutokana na mashambulizi ya waasi wa M23, msaada ambao utawasaidia kujenga upya maisha yao na njia zao za kujipatia riziki.  Katika makala leo Flo

  • UNDP yaomba msaada kusaidia wakimbizi wa ndani kujikwamua mashariki mwa DRC

    16/06/2025 Duración: 01min

    Huko jimboni Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, juhudi za kidiplomasia zinaendelea kumaliza mapigano, huko nalo shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP likitoa wito wa msaada kwa watu waliofurushwa makwao kutokana na mashambulizi ya waasi wa M23, msaada ambao utawasaidia kujenga upya maisha yao na njia zao za kujipatia riziki. Sharon Jebichii na taarifa zaidi

  • 13 JUNI 2025

    13/06/2025 Duración: 11min

    Katika Jarida la Umoja wa Mataifa leo Flora Nducha anakuleteaUmoja wa Mataifa walaani vikali mashambulizi ya Israel dhidi ya vinu vya nyuklia Jamhuri ya IranHuko Ituri Mashariki mwa DRC walinda amani wa Mpango wa Umoja wa Mataifa MONUSCO watoa huduma za afya kwa wananchiLeo ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu watu wenye Ualibino katika makala utamsikia mbunge kmwenye ualibino kutoka nchini TanzaniaNa mashinani utasiki ujumbe wa nini kifanyike kuhakikisha ndoto za watu wenye ulemavu zinatimia Afrika

  • Umoja wa Mataifa umefanya vema kuangazia saratani ya ngozi kwa wenye ualbino - Khadija Shaaban Taya (Keisha)

    13/06/2025 Duración: 03min

    Leo Ikiwa ni Siku ya Kimataifa ya Kuelimisha umma kuhusu Ualbino, Anold Kayanda wa idhaa hii anazungumza na Khadija Shaaban Taya almaarufu Keisha, Mbunge katika Bunge la Tanzania alipohudhuria mkutano wa mkataba wa watu wenye ulemavu uliofanyika wiki hii hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani. Keisha anaanza kwa kueleza anavyoithamini siku ya leo.

  • Pamoja na ulinzi wa raia, walinda amani wa UN Ituri waendesha kampeni ya afya..

    13/06/2025 Duración: 01min

    Huko jimboni Ituri, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Bangladesh wameendesha kampeni ya afya na kusaidia wakimbizi wa ndani kupata matibabu katika eneo hilo lililogubikwa na mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa waasi. Assumpta Massoi anasimulia zaidi.

  • Mashambulizi ya Israeli dhidi ya Iran, yalaaniwa vikali na UN..

    13/06/2025 Duración: 02min

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amelaani mashambulizi ya kijeshi yaliyofanywa na Israel dhidi ya vituo vya nyuklia vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, akionya juu ya hatari ya kuongezeka kwa mvutano katika eneo la Mashariki ya Kati huku mkuu wa wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA), Rafael Mariano Grossi amesema wanafanya tathimini athari za mashambulizi hayo katika vinu vya nyuklia Iran. Sharon Jebichi na taarifa kamili

  • Jifunze Kiswahili: Maana ya maneno "MBEUZI, MNYWANYWA NA MACHAGU.”

    12/06/2025 Duración: 54s

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya maneno "MBEUZI, MNYWANYWA NA MACHAGU.”

  • 12 JUNI 2025

    12/06/2025 Duración: 09min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kupinga utumikishaji wa watoto ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, ILO, linasema maudhui ni Maendeleo yako dhahiri, lakini bado kuna mengi ya kufanya: Hebu tuongeze kasi. Tunakupeleka nchini Tanzania kumulika harakati za kuwaepusha watoto kutumikishwa.Watu waliolazimika kukimbia makazi yao kutokana na vita, ukatili na mateso duniani kote imefikia kiwango cha juu kisichovumilika, hasa wakati huu ambapo ufadhili wa misaada ya kibinadamu unapungua kwa kasi. Kwa mujibu wa Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi UNHCR iliyotolewa leo kuhusu mwelekeo wa Ulimwengu, kufikia mwisho wa Aprili mwaka huu, kulikuwa na watu milioni 122.1 waliolazimika kuhama kwa nguvu, ikilinganishwa na watu milioni 120 mwaka uliopita katika kipindi kama hicho.Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya kupinga ajira kwa watoto, utafiti uliofanywa na mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la kazi duniani, ILO na la kuhudumia Watoto UNICEF

  • Masuala ya watu wenye ulemavu ni lazima yapewe nafasi kimataifa: Jakeel D. Abdullah

    11/06/2025 Duración: 01min

    Katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Kikao cha 18 cha Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu COSP18, kinaendelea na mwaka huu, mada kuu ni kuongeza uelewa wa haki na mchango wa watu wenye ulemavu katika maendeleo ya kijamii. Miongoni mwa washiriki ni ya kijana kutoka Louisiana, hapa  Marekani. Je amesema nini? Flora Nducha na taarifa zaidi

  • Akili Mnemba (AI) au teknolojia inaweza kuwasaidia watu wenye ulemavu – Bongani Simphiwe Makama

    11/06/2025 Duración: 03min

    Kikao cha 18 cha Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu – COSP18 – kinaendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ikiangazia juhudi za kimataifa za kuhakikisha usawa na ujumuishaji kwa watu wenye ulemavu. Miongoni mwa washiriki ni Bongani Simphiwe Makama mwakilishi wa watu wenye ulemavu kutoka Ufalme wa Eswatini, ambaye amepata nafasi ya kuzungumza na Idhaa ya Kiswahili kuhusu uzoefu wake, yale aliyojifunza, na changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu nchini kwake. Sharon Jebichii na Makala zaidi.

  • 11 JUNI 2025

    11/06/2025 Duración: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia ajali mbayá ya meli katika pwani ya Djibouti lililokuwa linabeba wahamiaji wengi. Pia tunasalia hapa makao makuu ambapo Kikao cha 18 cha Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu COSP18. Mashinani tutakwenda nchini DRC.Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, (IOM) kwa ushirikiano wa karibu na mamlaka za Djibouti, linaongeza juhudi zake za kibinadamu kufuatia tukio la kusikitisha lililotokea pwani ya Djibouti ambapo takriban wahamiaji wanane walikufa maji na wengine 22 hawajulikani walipo.Katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Kikao cha 18 cha Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu COSP18, kinaendelea na mwaka huu, mada kuu ni kuongeza uelewa wa haki na mchango wa watu wenye ulemavu katika maendeleo ya kijamii. Miongoni mwa washiriki ni ya kijana kutoka Louisiana, hapa  Marekani.Makala tutasalia hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani ambapo Kikao cha 18 cha Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu

  • IOM yachukua hatua za dharura baada ya wahamiaji kufa maji katika pwani ya Djibouti

    11/06/2025 Duración: 01min

    Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, (IOM) kwa ushirikiano wa karibu na mamlaka za Djibouti, linaongeza juhudi zake za kibinadamu kufuatia tukio la kusikitisha lililotokea pwani ya Djibouti ambapo takriban wahamiaji wanane walikufa maji na wengine 22 hawajulikani walipo. Anold Kayanda na maelezo zaidi.

  • 10 JUNI 2023

    10/06/2025 Duración: 10min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika ukanda wa Gaza, huko mashariki ya Kati kwenye eneo la Palestina lialokaliwa kimabavu na Israeli ambapo vinazidi kuibua changamoto mpya kila uchao.Changamoto ya uzazi duniani si kuhusu watu kukataa kuwa wazazi ni kuhusu kunyimwa fursa ya kuchagua kuwa mzazi imesema ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA iliyotolewa leo na kuonesha kuwa kuwa matatizo ya kiuchumi, ukosefu wa usawa wa kijinsia, na hofu kuhusu maisha ya baadaye vinawazuia mamilioni ya watu kupata familia wanazotamani.Tishio la baa la njaa linaendelea kuiandama Sudan iliyoharibiwa vibaya na vita, limeonya leo Shirika laUmoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP, likitoa wito wa dharura kwa jamii ya kimataifa kusaidia kukidhi mahitaji yanayoongezeka na kuzuia maafa zaidi ya kibinadamu.Kwa mara ya kwanza dunia inaadhimisha siku ya kimataifa ya Mazungumzo baina ya Ustaarabu tofauti yenye lengo la kuchagiza amani, maelewano na mshikamano k

  • UNEP inashirikiana na taifa la Tanzania kupambana na taka za plastiki - Clara Makenya

    09/06/2025 Duración: 06min

    Mkutano wa tatu wa Umoja wa Mataiifa kuhusu Bahari UNOC3 ukiendelea mjini Nice, Ufaranzsa, tunakuletea mahojiano kati ya Nafisa Didi afisa habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania UNIC Dar es salaam na Clara Makenya, Mkuu wa Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira UNEP nchini Tanzania na Afisa Mawasiliano wa shirika hilo kwa Namibia, wakimulika mchango wa UNEP katika kuzisaidia nchi kupambana na taka za plastiki ambayo ni mada kuu ya mkutano wa UNOC3.

  • Mustakabali wa bahari u mikononi mwetu sisi tunaoiharibu - UN

    09/06/2025 Duración: 02min

    Mkutano wa tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu bahari umeanza leo huko Nice nchini Ufaransa ambapo Katibu Mkuu wa Umoja huo António Guterres bila kumung’unya maneno ameelezea bayana jinsi binadamu anavyozidi kuhatarisha ustawi wa bahari lakini akionesha matumaini ya hali bora ya bahari iwapo hatua zitachukuliwa kwa maslahi ya binadamu na viumbe vya baharini. Assumpta Massoi amefuatilia na kuandaa taarifa hii.

  • 09 JUNI 2025

    09/06/2025 Duración: 11min

    Hii leo jaridani tunaangazia Mkutano wa tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu bahari umeanza leo huko Nice nchini Ufaransa, na masuala ya baharini ikiwa ni pamoja na uvuvi nchini Sao Tome, umuhimu wa kutunza mazingira nchini Kenya na uondoaji wa taka za plastiki Tanzania.Mkutano wa tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu bahari umeanza leo huko Nice nchini Ufaransa ambapo Katibu Mkuu wa Umoja huo António Guterres bila kumung’unya maneno ameelezea bayana jinsi binadamu anavyozidi kuhatarisha ustawi wa bahari lakini akionesha matumaini ya hali bora ya bahari iwapo hatua zitachukuliwa kwa maslahi ya binadamu na viumbe vya baharini.Nchini São Tomé na Príncipe, nchi ya visiwa viwili vidogo huko Afrika ya Kati, mpango wa FISH4ACP unaoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO unalenga kusaidia wavuvi na wauzaji samaki hasa wanawake na vijana kuongeza kipato na manufaa ya kijamii kwa njia endelevu huku wakipunguza athari mbaya kwa makazi ya asili na viumbe wa baharini. Paola Afè Do Espiritu Afonso ni miongon

  • São Tomé na Príncipe: Viumbe wa bahari, samaki, ni chanzo cha mapato, kuinua jamii na kuondoa umaskini

    09/06/2025 Duración: 02min

    Nchini São Tomé na Príncipe, nchi ya visiwa viwili vidogo huko Afrika ya Kati, mpango wa FISH4ACP unaoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO unalenga kusaidia wavuvi na wauzaji samaki hasa wanawake na vijana kuongeza kipato na manufaa ya kijamii kwa njia endelevu huku wakipunguza athari mbaya kwa makazi ya asili na viumbe wa baharini. Paola Afè Do Espiritu Afonso ni miongoni mwa wanawake wanaonufaika, Sharon Jebichi na maelezo zaidi.

  • Jifunze Kiswahili: maana ya neno KIHEREHERE

    05/06/2025 Duración: 45s

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno KIHEREHERE.

  • 05 JUNI 2025

    05/06/2025 Duración: 11min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo leo ikiwa ni siku ya mazingira duniani mwaka ikibeba maudhui “Tokomeza taka za Plastiki,” tunakwenda Tanzania kumsikia Clara Makenya, Mkua wa UNEP nchini humo na afisa mawasiliano wa shirika hilo kwa ajili ya Namibia akizungumza kuhusu changamoto ya taka za plastiki Tanzania na nini kifanyike kuzitokomeza.Naanzia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani ambapo leo kumefanyika tukio maalum la kukumbuka na kuenzi watumishi 168 wa Umoja wa Mataifa waliopoteza maisha wakitekeleza majukumu yao ya ulinzi wa amani, haki, na usaidizi, Mishumaa iliwashwa na kisha walitajwa majina yao mmoja baada ya mwingine akiwemo Nats.. mlinda amani wa UN kutoka Tanzania. Wanafamilia walipokea tuzo maalum za kutambua mchango wao.Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya mazingira, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametaka hatua za dharura kutokomeza janga la uchafuzi utokanao na taka za plastiki, akilitaja kama “janga” linaloikaba dunia na kutishia afya ya binad

  • Uwekezaji sahihi ni ule unaoanzia kwa wananchi na si ngazi ya juu - Madina

    04/06/2025 Duración: 02min

    Mkutano wa siku mbili kuhusu Ubia wa Kimataifa kwa ajili ya dunia endelevu umekunja jamvi huko Hamburg nchini Ujerumani ambako Balozi wa Mabadiliok ya Tabianchi wa Vijana wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Tanzania, Madina Jubilate Kimaro ameshiriki. 

página 3 de 5