Habari Za Un
16 JUNI 2025
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editor: Podcast
- Duración: 0:09:59
- Mas informaciones
Informações:
Sinopsis
Hii leo jaridani tunaangazia baa la njaa katika nchi 13 duniania amabzo hakuna uhakika wa chakula, na hali ya kibinadamu kwa wakimbizi wa DRC. Makala tunasalia hapa makao makuu na mashinani tunakwenda nchini Nepal, kulikoni?Ripoti mpya ya pamoja ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo jijini Roma, Italia inatahadharisha kuwa watu katika nchi 5 kati ya nchi 13 zenye njaa duniani wako kwenye hatari kubwa ya kukumbwa na njaa kali, vifo na maafa ikiwa msaada wa kibinadamu hautatolewa haraka na juhudi za kimataifa hazitaelekezwa kukomesha migogoro, kupunguza ufurushwaji na kuongeza msaada wa haraka kwa kiwango kikubwa.Huko jimboni Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, juhudi za kidiplomasia zinaendelea kumaliza mapigano, huko nalo shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP likitoa wito wa msaada kwa watu waliofurushwa makwao kutokana na mashambulizi ya waasi wa M23, msaada ambao utawasaidia kujenga upya maisha yao na njia zao za kujipatia riziki. Katika makala leo Flo