Sinopsis
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Episodios
-
Grandi: Msaada wa haraka unahitajika DRC wakati wakimbizi wanaendelea kufungasha virago
25/10/2024 Duración: 01minWakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wanaendelea kukimbilia Uganda kukwepa machafuko nchini mwao, huku rasilimali zikikaribia kikomo. Ameonya Kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Filippo Grandi, akiwa ziarani nchini Uganda hivi karibuni kwenye kambi inayohifadhi wakimbizi wa DRC na kutoa wito kwa jamii ya kimataifa kuongeza msaada.Wakimbizi wanaokimbia mzozo nchini DRC wanashuhudia matukio ya kutisha ya mauaji na ubakaji amesema Grandi, alipotembelea kambi ya ......aliyetembelea kambi za wakimbizi, Uganda na kusimuliwa hadithi za uchungu mkubwa“Sijawahi kusikia simulizi za machungu na hofu kama hizi za mauaji, ubakaji wa watoto mbele ya mama zao, wanawake wajawazito kukatwa vipande na makundi yenye silaha, na hofu kutawala maeneo yote ya Mashariki mwa Congo.”Kutokana na hali hii, Grandi anasema amani ndiyo inahitajika zaidi kwa sasa ili kumaliza dhuluma zinazowakumba wakimbizi wa Congo.“Ni wakati sasa jamii ya kimataifa ijitolee kwa
-
25 OKTOBA 2024
25/10/2024 Duración: 09minHii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na ujumbe wa Filippo Grandi wa UNHCH ambaye yuko ziarani Uganda. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini DRC, kulikoni?Hali Gaza inaendelea kuwa tete wakati ucheleweshwji wa kuhamisha wagonjwa hususan watoto wanaohitaji msaada wa haraka wa huduma za afya imekuwa ni hukumu ya kifo kwao huku maelfu ya watu wakiendelea kukosa mahitaji ya muhimu ya kila siku ikiwemo chakula kama mkate, yameonya leo mashirika ya Umoja wa Mataifa.Wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wanaendelea kukimbilia Uganda kukwepa machafuko nchini mwao, huku rasilimali zikikaribia kikomo. Ameonya Kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mtaifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Filippo Grandi, akiwa ziarani nchini Uganda hivi karibuni kwenye kambi inayohifadhi wakimbizi wa DRC na kutoa wito kwa jamii ya kimataifa kuongeza msaada, kama inavyoeleza taarifa ya Bosco Cosmas.Makala inayotupeleka Nairobi Kenya kwake Stella Vuzo afisa habari wa kitengo
-
UN: Hali si hali tena Gaza vifo vyatawala hospitali na kwa raia hata mkate ni adimu kupatikana
25/10/2024 Duración: 01minHali Gaza inaendelea kuwa tete wakati ucheleweshwji wa kuhamisha wagonjwa hususan watoto wanaohitaji msaada wa haraka wa huduma za afya imekuwa ni hukumu ya kifo kwao huku maelfu ya watu wakiendelea kukosa mahitaji ya muhimu ya kila siku ikiwemo chakula kama mkate, yameonya leo mashirika ya Umoja wa Mataifa.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limeonya kwamba idadi ya watoto wanaohamishwa Gaza kwa ajili ya huduma za dharura za matibabu imeshuka sana hadi kufikia mtoto mmoja kwa siku na kusema kiwango hiki kikiendelea itachukua zaidi ya miaka 7 kuhamisha watoto 2500 wanaohitaji huduma ya dharura ya matibabu.Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswis msemaji wa UNICEF James Elder amesema “matokeo yake watoto wanakufa Gaza sio tu kutokana na mabomu na risasi na makombora yanayofurusmishwa lakini kwa sababu hata kama miujiza inatokea , hata kama mabomu yanalipuka na nyumba kuporomoka, na vifo kuongezeka watoto wananusurika, lakini kisha wanazuiliwa kuondoka Gaza Kwenda kupokea huduma
-
24 OKTOBA 2024
24/10/2024 Duración: 11minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina mada inayotupeleka nchini Kenya kuzunguza na uongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu mada tofauti ikiwemo uwakilishi wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno HEKEMUA.Uchambuzi mpya wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) uliotolewa leo jijini New York, Marekani katika Siku ya Kimataifa ya Polio, unaonesha kwamba asilimia 85 ya watoto 541 waliokumbwa na polio duniani mwaka wa 2023 wanaishi katika nchi 31 zenye mifumo dhaifu, zinazokabiliwa na mizozo, halikadhalika zilizo hatarini.Umoja wa Mataifa ulijengwa na ulimwengu, kwa ajili ya ulimwengu, ndivyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, alivyouanza ujumbe wake mahususi kwa ajili ya siku ya leo ya Umoja wa Mataifa.Na leo Oktoba 24 huko Kazan nchini Urusi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amehutubia mkutano wa viongozi wa kundi la BRICS yaani Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini akisisit
-
Jifunze Kiswahili - maana ya neno HEKEMUA!
24/10/2024 Duración: 22sKatika kujifunza lugha ya Kiswahili leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno HEKEMUA!
-
23 OKTOBA 2024
23/10/2024 Duración: 10minHii leo jaridani tunaangazia mashambulizi ya Israeli kaskazini mwa Gaza unaoleta changamoto za kuendelea na chanjo ya polio, na virusi vya Marburg nchini Rwanda. Makala tunakupeleka nchini Uganda na mashinani nchini Lebanon, kulikoni?Mashambulizi makali ya anga kutoka kwa jeshi la Israel, idadi kubwa ya watu kutawanywa na ukosefu wa fursa ya kufika Gaza Kaskakzini vimelazimisha kuahirishwa kwa kameni ya chanjo kwa mujibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Afya Duniani WHO, la kuhudumia watoto UNICEF na la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWAMkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani amewapongeza wahudumu wa afya wa nchini Rwanda kwa kazi kubwa wanaoyoifanya kukabiliana na ugonjwa wa Marburg. Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus ameeleza hisia zake hizo mwishoni mwa wiki alipofanya ziara katika vituo mbalimbali vya afya katika mji Mkuu wa nchi hiyo, Kigali.Ndoa za utotoni,ubakaji na kutelekeza watoto, haya ndio matatizo yaliyokuwa yanaripotiwa mara nyingi zaidi kwa kuathiri watoto kat
-
Mbinu bora za malezi zimebadilisha maisha katika Wilaya ya Kyegegwa - UNICEF Uganda
23/10/2024 Duración: 03minNdoa za utotoni,ubakaji na kutelekeza watoto, haya ndio matatizo yaliyokuwa yanaripotiwa mara nyingi zaidi kwa kuathiri watoto katika makazi ya wakimbizi katika wilaya Kyegegwa magharibi mwa Uganda. Hata hivyo, kwa msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto UNICEF na ufadhili kutoka wahisani wa Uingereza UKaid, maelfu ya wazazi katika makazi ya wakimbizi na jamii zinazohifadhi waakimbizi katika wilaya ya Kyegegwa wamepewa mafunzo juu ya malezi bora ili kuondoa ukatili dhidi ya watoto, wanawake, na wasichana. Leo tuko katika wilaya ya Kyegegwa nchini Uganda ambapo, kwa msaada wa UNICEF, wafanyakazi wa kijamii, kamati za ulinzi na ustawi wa watoto, na kikosi cha polisi; wote wamepewa mafunzo mwafaka ili kuhakikisha ulinzi wa watoto unaofaa na wa kudumu, na tunakutana na Agnes Karungi mama mwenye umri wa miaka ishirini na mmoja wa wanufaika wa mradi wa malezi bora. Mbali na kukumbana na changamoto za kuwa mama kijana, mwanaye Agnes, ni mwenye ulemavu na zaidi ya hayo a
-
UN: Mashambulizi ya anga ya Israel yalazimisha kampeni ya chanjo kusitishwa Gaza Kaskazini
23/10/2024 Duración: 02minMashambulizi makali ya anga kutoka kwa jeshi la Israel, idadi kubwa ya watu kutawanywa na ukosefu wa fursa ya kufika Gaza Kaskakzini vimelazimisha kuahirishwa kwa kameni ya chanjo kwa mujibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Afya Duniani WHO, la kuhudumia watoto UNICEF na la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA. Asante Anold, kampeni hiyo iliyoahirishwa ilitakiwa kuanza leo n ani duru ya mwisho ya chango ya kampeni iliyolenga kuwachanja watoto 119,279 kote Gaza Kaskazini kwa dozi ya pili ya chanjo ya polio aina ya nOPV2, lakini hali ya sasa imefanya iwe vigumu kwa familia kupeleka watoto wao kwenye vituo vya chanjo, na kwa wahudumu wa afya kuendesha huduma kwa usalama.Mashambulizi ya makombora yanayoendelea dhidi ya miundombinu ya kiraia yamepunguza maeneo yanayokubaliwa kwa usitishaji wa uhasama kwa mnajili ya masuala ya kibinadamu kuwa kwenye Jiji la Gaza pekee, ikilinganishwa na wakati wa awamu ya kwanza ya chanjo iliyofanyika tarehe 1-12 Septemba 2024.Hali hii inahatarisha kufikiwa kwa le
-
Dkt. Tedros: Heshima kwa wahudumu wa afya wa Rwanda wanavyopambana na Marburg
23/10/2024 Duración: 01minMkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani amewapongeza wahudumu wa afya wa nchini Rwanda kwa kazi kubwa wanaoyoifanya kukabiliana na ugonjwa wa Marburg. Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus ameeleza hisia zake hizo mwishoni mwa wiki alipofanya ziara katika vituo mbalimbali vya afya katika mji Mkuu wa nchi hiyo, Kigali."Ninawapongeza wahudumu wa afya waliojitolea ambao wamejiweka hatarini kuokoa wenzao, na ambao wameendelea kufanya kazi licha ya hatari. Na ninaenzi wale ambao tumewapoteza."Pia Dkt. Tedros akaeleza kuwa yeye na wenzake wamefurahishwa na namna ya utoaji huduma ambayo haijawahi kutumiwa katika mlipuko ya magonjwa ya namna hii barani Afrika akitolea mfano wagonjwa wawili aliowashuhudia wakiendelea vizuri kwamba waliokolewa kwa kuwekewa mipira iliyopeleka hewa ndani ya mwili.“Tunaamini hii ni mara ya kwanza kwa wagonjwa wenye virusi vya Marburg barani Afrika kuingiziwa na kutolewa mpira wa hewa. Wagonjwa hawa wangefariki dunia katika milipuko ya hapo awali. Hii inaonesha kazi a
-
Kuanza tena kwa shughuli za Redio RTNC kutawawezesha kupigana dhidi ya taarifa potofu na za uongo - MONUSCO
22/10/2024 Duración: 05minUmoja wa Mataifa unaendelea kuunga mkono serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC katika kukabili habari potofu na za uongo hususan huko mashariki mwa nchi ambako vikundi vilivyojihami vinaendelea kushambulia raia na kupambana na jeshi la serikali. Hivi karibuni Umoja wa Mataifa kupitia ujumbe wake wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, umeipatia kituo cha Taifa cha Redio na Televisheni, RTNC huko Beni jimboni Kivu Kaskazini jengo na vifaa vyenye thamani ya takriban dola elfu hamsini za Kimarekani. Hatua hiyo iliwezesha RTNC kuanza tena matangazo yake. Mwandishi wetu wa DRC, George Musubao alifika kituoni hapo kuzungumza na wahusika na wanufaika.
-
22 OKTOBA 2024
22/10/2024 Duración: 09minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini DRC kufuatilia kazi za kituo cha Taifa cha Redio na Televisheni, RTNC huko Beni jimboni Kivu Kaskazini za kakabiliana na habari potofu. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani.Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo mjini Cairo, Misri, imebainisha kwamba athari za vita zimerudisha nyuma maendeleo huko Gaza kwa takriban miaka 69. Ripoti hiyo iliyoratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP na Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Kiuchumi na Kijamii kwa Asia Magharibi imeonya kwamba bila kuondoa vikwazo vya kiuchumi na kuwekeza katika maendeleo, uchumi wa Palestina unaweza kushindwa kurejesha viwango vya kabla ya vita na kusonga mbele kwa kutegemea misaada ya kibinadamu pekee.Kiongozi wa timu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) ya kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa Marburg Dkt. Janet Diaz ameeleza kwamba uongozi thabiti wa serikali ya Rwanda umewezesha kufanya uamuzi wa haraka na kuchukua
-
Nadipo: Asante WFP kwa mradi wa mizinga ya nyuki sasa familia yangu inatabasamu
21/10/2024 Duración: 03minKaunti ya Turkana Kaskazini mwa Kenya moja ya maeneo kame mradi wa ufugaji nyuki wa WFP umekuwa mkombozi kwa wakulima walioathirika na mabadiliko ya tabianchi.Katika kaunti hii vumbi linalotimuka katika eneo tambarare lisilo na miti linakufanya kujiuliza je Nini kizuri kinaweza kufanyika hapa kwenye ukame uliotamalaki? Lakini cha kustaajabisha ni kwamba kwa kuwezeshwa mengi yanawezekana ikiwemo njia bora za kuhakikisha uhakika wa chakula na hata kubadili maisha ya watu kama anavyosema mkulima wa nyuki Nadipo Lotelei mnufaika wa mradi wa mizinga ya nyuki kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP. “Hatua iliyochukuliwa na WFP kutupatia mizinga ya nyuki imekuja kama nyota ya jaha kwangu kwa sababu siwezi kutembea umbali mrefu kutokana na ajali niliyopata. Mradi huu umenisaidia sana mimi ili kuweza kusaidia watoto wangu na mke wangu. Mke wangu ameweza kuanzisha biashara ya duka kutokana na faida niliyopata ambayo sasa inatumika kama chnzo cha kipato cha mahitaji ya kaya yetu.”
-
Mlo shuleni ulibadilisha maisha yangu- Mkurugenzi wa WFP Somalia
21/10/2024 Duración: 01minKila siku, mamilioni ya watoto kote ulimwenguni huenda shule wakiwa na njaa, wengi wao wakiteseka na utapiamlo sugu ambao huathiri ukuaji wa kiakili na utendaji wao katika masomo. Wanaobahatika huweza tu kumaliza masomo yao na kufanikiwa maishani kutokana na programu ya ‘mlo ya shuleni’ inayoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula Duniani (WFP). Mfano wa wanufaika hao ni El-Khidir Daloum, Mkurugenzi wa sasa wa WFP nchini Somalia. "Mimi ni zao la mlo wa shule," hayo ni maneno ya El-Khidir Daloum ambaye ana shukrani tele kwa WFP kwa kuendesha programu ya ‘mlo shuleni’ iliyomfaidisha alipokuwa mwanafunzi. Hivi sasa, akiwa Mkurugenzi wa WFP nchini Somalia, Daloum ameweka dhamira ya kazi yake kuhakikisha upatikanaji wa chakula kwa wote. Je Daloum aliifahamu vipi programu ya mlo shuleni ya WFP kwa mara ya kwanza?“Tulipofika pale, tukakuta ni shule ya bweni, wakati huo wazazi wetu hawangeweza kugharamia shule hiyo. Kwa hivyo, shule ilifanya ushirikiano kati ya serikali na Sh
-
21 OKTOBA 2024
21/10/2024 Duración: 09minHii leo jaridani tunaangazia mkutano wa COP16 katika mji wa Santiago de Cali au Cali huko nchini Colombia na ufugaji nyuki Turakana nchini Kenya. Pia tunakupeleka nchini Somalia kufutilia programu wa WFP wa mlo shuleni na mashinani inatupeleka nchini Lebanon.Mkutano wa 16 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa bayonuai (COP16) umeng’oa nanga leo katika mji wa Santiago de Cali au Cali huko nchini Colombia ambapo mataifa 196 yatajadili jinsi ya kusitisha na kubadili mwelekeo wa kudorora kwa ulimwengu wa asili.Kila siku, mamilioni ya watoto kote ulimwenguni huenda shule wakiwa na njaa, wengi wao wakiteseka na utapiamlo sugu ambao huathiri ukuaji wa kiakili na utendaji wao katika masomo. Wanaobahatika huweza tu kumaliza masomo yao na kufanikiwa maishani kutokana na programu ya ‘mlo ya shuleni’ inayoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula Duniani (WFP). Mfano wa wanufaika hao ni El-Khidir Daloum, Mkurugenzi wa sasa wa WFP nchini Somalia.Makala inatupeleka Kaunti ya Turkana Kaskazini mwa
-
COP16: Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Baionuai waanza nchini Colombia
21/10/2024 Duración: 01minMkutano wa 16 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa bayonuai (COP16) umeng’oa nanga leo katika mji wa Santiago de Cali au Cali huko nchini Colombia ambapo mataifa 196 yatajadili jinsi ya kusitisha na kubadili mwelekeo wa kudorora kwa ulimwengu wa asili. COP16 kwa siku 12, viongozi na wadau kutoka kote duniani wanatarajiwa kujadili namna ya wanadamu kuishi kwa amani na asili ya ulimwengu, kama wasemavyo nchi mwenyeji Colombia kwa lugha ya kihispanyola Paz con la Naturaleza yaani amani na asili.Washiriki, kwa kina watajadili utekelezaji wa mkakati wa Kimataifa wa Kunming-Montreal kuhusu bayoanuai, makubaliano ya kihistoria ya mwaka 2022 ya kusitisha na kubadili upotevu wa asili. Pia watachunguza jinsi ya kuelekeza mabilioni ya dola kwa nchi zinazoendelea ili kuhifadhi na kudhibiti bioanuai kwa uendelevu. Na watajadili sheria za msingi ambazo zinaweza kuhitaji kampuni za kibinafsi kufidia mataifa.Katika sherehe za ufunguzi wa mkutano huu hapo jana, kwa njia ya video, Katibu Mkuu wa
-
Nchi zote pamoja na mashirika ya kimataifa ikiwemo UN yanawajibika kukomesha ukaliwaji wa Palestina
18/10/2024 Duración: 02minTume hiyo huru imeyasema hayo katika taarifa mpya ya msimamo wa kisheriia iliyotolewa mjini Geneva Uswis kuhusu eneo linalokaliwa la Palestina ikiwemo Jerusalem Mashariki ambayo imeweka wazi maoni ya tume kuhusiana na wajibu wa serikali na jinsi Baraza Kuu na Baraza la Usalama linavyoweza kutambua na kutekeleza mbinu na hatua sahihi zinazohitajika kwa kazi hiyo hadi mwisho wa ukaliwaji huo, na kwa haraka iwezekanavyo.Tume ihiyo imebaini kwamba maoni ya ushauri ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki kuhusu matokeo ya Kisheria yanayotokana na sera na desturi za Israel katika eneo linalokaliwa la Palestina ikiwa ni pamoja na Jerusalem Mashariki ni wenye mamlaka na usio na utata kwa kusema kwamba kuendelea kuwepo kwa Israel katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu ni kinyume cha sheria na sheria ya kimataifa.Taarifa hiyo ikitolewa Geneva Gaza kwenyenyewe hali inaendelea kuwa tete, kwa mujibu wa Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestinna UNRWA Phillipe Lazzarini, kwani shule nyin
-
Mbegu za asili zinanisaidia kukabili mabadiliko ya tabianchi - Mkulima
18/10/2024 Duración: 03minShirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO linapigia chepuo uwepo wa mifumo ya uzalishaji chakula inayoendana na kila eneo husika, mathalani kilimo kitumie mbegu za asili za eneo husika kama mbinu ya kukabili mabadiliko ya tabianchi. Kupata aina tofauti tofauti za mbegu za asili kwa eneo husika kunainua kipato cha wakazi wa vijijini na kuongeza mnepo majanga yanapotokea. Na hicho ndio anafanya mkulima kutoka Tanzania ambaye wakati wa maonesho ya siku ya chakula duniani huko mkoani Kagera, kaskazini magharibi mwa Tanzania alieleza kwa nini ameamua kuchukua hatua hiyo. Assumpta Massoi anasimulia zaidi.
-
UN Ripoti: Uwezekano wa kifo cha Dag Hammarskjöld kuwa ni hila unaongezeka kutokana na taarifa mpya
18/10/2024 Duración: 02minRipoti nyingine mpya ya tathimini ya uchunguzi wa hali na mazingira ya kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka 1961 Dag Hammarskjöld imetolewa leo ikiwa na vipengele vinne vipya vikiongeza uwezekano kwamba kifo hicho cha ajali ya ndege kilikuwa ni hila. Asante Anold kwanza ikumbukwe kuwa hii sio ripoti ya kwanza na huenda isiwe ya mwisho ya kutathimini hali na mazingira yliyochangia ajali ya ndege iliyokatili maisha ya Dag Hammarskjöld tarehe 17 Septemba 1961 akiwa njia kuelekea Congo ambayo sasa ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Cngo DRC, kujadili usitishwaji wa uhasama ila ni ripoti ya karibuni zaidiRipoti inasema mwenyekiti wa jopo la tathimini ya uchunguzi jaji mkuu wa zamani wa Tanzania Mohamed Chande Othman amepokea taarifa mpya muhimu kutoka kwa nchi wanachama ambazo zinajumuisha maeneo haya Mosi: uingiliaji unaowezekana wa Nchi Wanachama wa mawasiliano husika.Pili: Uwezo wa wanajeshi wa Katanga, au wengine, wa kufanya shambulio linalowezekana kwenye ndege ya SE-BDY,Tatu: kuwepo
-
18 OKTOBA 2024
18/10/2024 Duración: 10minHii leo jaridani tunaangazia eneo linalokaliwa kwa mbavu la Kipalestina, na ndoto Mchezaji kijana wa soka zilizokatizwa na vita katika ukanda wa Gaza. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani Kenya, kulikoni?Tume Huru ya Kimataifa ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa kuhusu eneo linalokaliwa la Palestina leo imesema mataifa yote na mashirika ya kimataifa, ikiwa ni amoja na Umoja wa Mataifa, wana wajibu chini ya sheria za kimataifa wa kukomesha uwepo haramu wa Israel katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu, wakati mashambulizi Gaza yakishika kazi na kuongeza madhila kwa raia.Katika ufukwe wa Al- Mawasi, magharibi mwa mji wa Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza huko Mashariki ya Kati, mchezaji mpira wa Klabu ya Soka ya Rafah Services anaendelea na mazoezi yake ili kuendeleza uthabiti wa mwili kama mchezaji wa soka wa kulipwa wa klabu hiyo muhimu wakati huu mashambulizi ya makombora yakiendelea kwenye eneo hilo.Makala inatupeleka Tanzania hususan mkoani Kagera, kaskazini magharibi mwa taifa hilo la Afri
-
Mohamed hajakata tamaa ya kuwa mwanasoka maarufu - Gaza
18/10/2024 Duración: 01minKatika ufukwe wa Al- Mawasi, magharibi mwa mji wa Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza huko Mashariki ya Kati, mchezaji mpira wa Klabu ya Soka ya Rafah Services anaendelea na mazoezi yake ili kuendeleza uthabiti wa mwili kama mchezaji wa soka wa kulipwa wa klabu hiyo muhimu wakati huu mashambulizi ya makombora yakiendelea kwenye eneo hilo. Jua linazama hapa kwenye ufukwe wa Al Mawasi, kwenye bahari ya Mediteranea, wengine wakiwa wanaogelea, na kwa mbali mahema ya waliosaka hifadhi baada ya kufurushwa kaskazini mwa Gaza, mmoja anaonesha mbwembwe za dana dana ya mpira, anajitambulisha."Naitwa Mohamed Abu Jalda, mchezaji wa Klabu ya Rafah Services katika daraja la kwanza. Nilikuwa na ari kubwa ya kuwa mchezaji mkubwa wa soka kama wengine walioko nje ya Ukanda wa Gaza, lakini kutokana na vita, tamaa yangu na maisha yangu yalicheleweshwa, sasa nina zaidi ya miaka 20, nikijaribu kuwa mchezaji wa soka, lakini siwezi kwa sababu naishi Gaza ambapo kuna mapigano ya mara kwa mara. Kila siku nahisi kama ninakufa; Mungu