Sbs Swahili - Sbs Swahili

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 107:39:45
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Listen to interviews, features and community stories from the SBS Radio Swahili program, including news from Australia and around the world. - Sikiza mahojiano, makala na hadithi za jumuiya kutoka Idhaa ya Kiswahili ya SBS Radio, ikijumuisha taarifa za habari kutoka Australia na ulimwenguni.

Episodios

  • Taarifa ya Habari 20 Februari 2025

    20/02/2025 Duración: 07min

    Mkuu wa shirika la usalama wa ndani nchini Australia ana onya, kuna ongezeko la wimbi la watoto wanao lengwa kutumia maudhui ya itikadi kali mtandaoni, na ame ongezea kuwa makampuni makubwa ya mtandao wakijamii yana nafasi kubwa yaku zuia shughuli hizo, kwa kutumia vifaa vinavyo wezesha bidhaa zao.

  • Jinsi ya kukabiliana na unyanyasaji shuleni au mtandaoni

    19/02/2025 Duración: 14min

    Kutoa mazingira salama na jumuishi ni dhamira ya msingi ya kila jumuiya ya shule ya Australia. Ila wazazi wanastahili fanya nini mtoto wao anapo nyanyaswa shuleni?

  • Taarifa ya Habari 18 Februari 2025

    18/02/2025 Duración: 21min

    Onyo limetolewa kuhusu matokeo ya kura ambayo matokeo hayo ya karibu huenda yasi mulike kura zawa Australia.

  • Uchomaji wakitamaduni: kutumia moto kulinda dhidi ya moto na kufufua Nchi

    18/02/2025 Duración: 15min

    Kuishi katika mazingira yenye moto kama Australia, wengi wetu hupata ugumu waku ona moto kama kitu kingine zaidi yakuwa tisho.

  • Taarifa ya Habari 17 Februari 2025

    17/02/2025 Duración: 08min

    Kiongozi wa upinzani wa shirikisho Peter Dutton amesema yuko tayari kufanya mazungumzo na wabunge huru, kama vyama viwili vikubwa nchini havita weza unda serikali ya wengi.

  • Taarifa ya Habari 13 Februari 2025

    13/02/2025 Duración: 06min

    Waziri wa Afya wa jimbo la New South Wales, ameomba msamaha jumuiya ya wayahudi baada ya video inayo zungushwa mtandaoni, kuwaonesha wauguzi wawili waliokuwa wakitoa vitisho kwa wagonjwa wenye asili ya Israel.

  • Dkt Damacent afunguka kuhusu umuhimu wakuwafanya vipimo vya tezi dume

    12/02/2025 Duración: 15min

    Wanaume mara nyingi hujipata katika hali tata kiafya kwa sababu ya kuchelewa kuchukua hatua zinazo faa kupata huduma.

  • Taarifa ya Habari 11 Februari 2025

    11/02/2025 Duración: 17min

    Kundi maarufu la madaktari limezindua mpango mpya kabla ya uchaguzi mkuu, kundi hilo limesema lita hakikisha upatikanaji kwa huduma yama GP kwa bei nafuu kwa kila mtu nchini Australia.

  • Jinsi ya kuandaa ombi la kazi

    11/02/2025 Duración: 10min

    Unapo ona tangazo la kazi linalo kuvutia, kuelewa hatua zinazo fuata ni muhimu.

  • Taarifa ya Habari 10 Februari 2025

    10/02/2025 Duración: 08min

    Hesabu zina endelea katika chaguzi dogo katika eneo bunge la Werribee ambalo liliwahi kuwa ngome ya chama cha Labor katika vitongoji vya magharibi ya mji wa Melbourne.

  • Nanga "Tutaweka polisi wa taifa, utawala, na mfumo wa haki”

    10/02/2025 Duración: 07min

    Waasi wa M23 wametangaza nia yao ya “kuikomboa Kongo yote” wakati wa mkutano wa hadhara mjini Goma.

  • Taarifa ya Habari 7 Februari 2025

    07/02/2025 Duración: 19min

    Serikali ya Wilaya ya Kaskazini ime fikia makubaliano ya thamani yama milioni ya dola na mashirika yawa Australia wa kwanza, kutoa huduma kwa maeneo ya vijijini.

  • Jinsi ya kupata Malipo ya Likizo ya Wazazi nchini Australia

    07/02/2025 Duración: 12min

    Nchini Australia, baadhi ya wazazi wanaweza pokea malipo ya likizo ya wazazi kutoka serikali na waajiri wao. Ila si kila mtu ana stahiki.

  • Taarifa ya Habari 6 Februari 2025

    06/02/2025 Duración: 07min

    Nchi zaki Arabu, Umoja wa Mataifa na washirika wakaribu wa Marekani wamekosoa pendekezo la Donald Trump kuchukua ukanda wa Gaza, naku tawanya wa Palestina kuwa hatua hiyo ita yumbisha kanda hiyo na kudhoufisha juhudi zakupata suluhu ya nchi mbili.

  • Taarifa ya Habari 4 Februari 2025

    04/02/2025 Duración: 19min

    Wanasiasa wame ashiria kufunguliwa kwa Bunge la taifa kwa kuhudhuria ibada katika Kanisa laki Katoliki la Mtakatifu Christopher, mjini Canberra leo asubuhi Jummanne 4 Feb 2025.

  • Ongezeko ya gharama ya shule yalazimisha baadhi ya familia kufanya maamuzi magumu

    04/02/2025 Duración: 09min

    Mwaka wa shule wa 2025 uli anza Jummanne 28 Januari katika majimbo ya Queensland na Kusini Australia, wanafunzi wa shule za msingi na upili walirejea shuleni Jumatano 29 Januari katika jimbo la Victoria na Wilaya ya Kaskazini.

  • Taarifa ya Habari 3 Februari 2025

    03/02/2025 Duración: 07min

    Waziri wa Kigeni Penny Wong amesema vikwazo vipya vya kufadhili ugaidi kwa mtandoa wa kundi lawa neo-Nazi wa mtandaoni kwa jina la Terrorgram, ni sehemu ya hatua za serikali dhidi ya mashambulizi dhidi ya ubaguzi wa wayahudi pamoja na uhalifu wa chuki.

  • Bw Omari "watu wana anza sema wakati wa Kabila ulikuwa afadhali kuliko sasa"

    03/02/2025 Duración: 11min

    Hali ya usalama inavyo zidi kudorora katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ndivyo serikali ya Rais Tshisekedi inavyo zidi kuwa chini ya shinikizo kubwa.

  • Taarifa ya Habari 31 Januari 2025

    31/01/2025 Duración: 18min

    Serikali ya shirikisho na Victoria zime tia saini mkataba wa uwekezaji wenye thamani ya dola bilioni $2.5 kwa elimu, ambayo serikali hizo zime sema uwekezaji huo utawasaidia wanafunzi, wafanyakazi pamoja na familia.

  • Rais Tshisekedi awarai vijana wajiunge na jeshi kupambana na M23

    31/01/2025 Duración: 06min

    Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Felix Tshisekedi, amewarai vijana kujiunga kwa wingi na jeshi la taifa kusaidia kupambana na waasi wa M23 wanaojaribu kukamata maeneo makubwa zaidi mashariki mwa nchi hiyo.

página 1 de 26