Sinopsis
Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.
Episodios
-
Kenya : Askofu wa kanisa katoliki walaani serikali
19/11/2024 Duración: 09minKatika makala tunajadili hatua ya viongozi wa dini nchini Kenya, kutuhumu serikali kwa kile wamedai imekuwa ikitoa ahadi za uongo kwa raia. Je unazungumziaje kauli hii ya viongozi wa dini nchini Kenya? Haya hapa maoni yako.
-
Sudan : IGAD yapendekeza vikosi kutuma kulinda raia
18/11/2024 Duración: 09minKwenye makala hayai tunajadili hatua ya Jumuiya ya IGAD kuripotiwa kupendekeza kutumwa kwa wanajeshi wa kulinda amani toka nchi za Afrika ambazo hazijajihusisha kwenye mzozo unaoendelea ili kusimamia mkataba wa usitishaji mapigano kati ya jeshi na wapiganaji wa RSF nchini #sudan. Unamtazamo gani kwa pendekezo hili? Haya hapa baadhi ya maoni yako.
-
Maoni ya wasikilizaji kuhusu matukio na habari juma lote ikiwemo COP29
15/11/2024 Duración: 10minMadu huru zilizoangaziwa na wasikilizaji wetu wiki hii
-
Australia imeridhia sheria kuwazuia watoto kutotumia mitandao ya kijamii
14/11/2024 Duración: 10minBunge la Australia limesema mitandao ya kijamii ina madhara makubwa kwa watoto
-
Australia yapitisha sheria ya kuwazuia watoto kutumia mitandao ya kijamii
14/11/2024 Duración: 10minBunge la Australia limesema mitandao ya kijamii ina madhara makubwa kwa watoto
-
Baraza la usalama limejadili mapendekezo ya Uingereza kuhusu mzozo wa Sudan
14/11/2024 Duración: 09minMapendekezo ya taifa la Uingereza yanataka vita kusitishwa nchini Sudan na kuruhusiwa misaada ya kibinadamu kuwafikia waathiriwa.
-
Changamoto zinazoandama mipango ya bima ya afya katika mataifa ya Afrika
12/11/2024 Duración: 10minNchini #kenya ,wagonjwa wengi wanaendelea kutaabika kupata huduma za afya kufuatia changamoto zinazotokana na utekelezwaji wa mpango mpya wa afya ,SHIF Hali hii ndiyo pia inayokumba nchi nyingi za Afrika zinazojaribu kutekeleza mipango ya afya inayosimamiwa na serikali.
-
Viwango vya umaskini nchini Uganda vimeongezeka mno ,yasema ripoti mpya
11/11/2024 Duración: 08minUmaskini umeendelea kukithiri katika baadhi ya maeneo nchini Uganda Ripoti ya shirika moja lisilo la kiserikali nchini #Uganda, inayoonesha kuwa karibu asilimia 68 ya raia nchini humo wanapata ugumu kujikimu kimaisha kutokana umasikini.
-
Maoni ya waskilizaji kuhusu taarifa zetu juma hili
09/11/2024 Duración: 09minKila Ijumaa rfi kiswahili inakupa nafasi kuchangia mada yoyote kuhusu taarifa zetu au kile kinachoendelea hapo ulipo. Haya ni maoni ya waskilizaji wetu juma hili.
-
Utekaji wakithiri kwa mataifa ya Africa Mashariki
07/11/2024 Duración: 09minKatika Makala haya, tunajadili hatua ya hivi karibuni ambapo baadhi ya mataifa ya Afrika Mashariki yamendelea kurekodi ongezeko la visa vya utekaji na mauaji, vingi vikitekelezwa na idara za usalama au watu wasiojulikana. Unazungumziaje hali hii ? Haya hapa baadhi ya maoni yako.
-
Donald Trump arejea White House kwa kishindo
07/11/2024 Duración: 10minDonald Trump amechaguliwa tena rais wa Marekani baada ya kukaa kwenye kijibaridi kwa kipindi cha miaka 4. Waskilizaji wa rfi Kiswahili walikuwa na maoni haya baada ya mshindi wa Trump.
-
Botswana : Chama tawala chasalimu amri
05/11/2024 Duración: 09minKatika makala haya tunajadili kilichotokea nchini Botswana ambapo Chama tawala Democratic Party, ambacho kimekuwa madarakani tangu enzi za ukombozi kwa maika 58, kimekubali kushindwa na kukabidhi madaraka kwa upinzani, Duma Boko akiapishwa kuhudumu rais kama rais wa sita wa Botswana. Je mataifa mengine ya Afrika yenye vyama vya ukombozi madarani yanaweza jifunza nini kutokana na uchaguzi wa Botswana?Ndilo swali Tumekuuliza na haya hapa baadhi ya maoni yako.
-
Africa: Uturuki yashiriki mkutano na Africa kuimarisha uhusiano
05/11/2024 Duración: 09minTaifa la Uturuki limefanya mkutano na viongozi wa Africa, nchi hiyo ikilenga kuimarisha uhusiano wake na Africa. Lakini je kuna la ziada katika mkutano huu. Haya hapa baadhi ya maoni yenu.
-
-
Kenya: pendekezo la kufanya marekebisho ya katiba kuongeza muda rais na wabunge madarakani
29/10/2024 Duración: 10min -
-
Kuongezeka kwa ubakaji dhidi ya wanawake na wasichana kwenye maeneo yenye mizozo
02/10/2024 Duración: 09min -
Ripoti yaonesha kushuka kwa uaminifu wa uchaguzi kati ya mwaka 2020 na 2024 katika nchi 21 Afrika
30/09/2024 Duración: 10min -
Kwa nini bado usawa wa kijinsia haujafikiwa katika mataifa mengi ya Afrika
26/09/2024 Duración: 09minRipoti ya hivi karibuni ya umoja wa mataifa ,kuhusu usawa wa kijinsia, takwimu zinaonesha hatua kupigwa lakini changamoto bado zimesalia.
-
Majengo duni yanayoporomoka na kusababisha majanga barani Afrika
25/09/2024 Duración: 09minWiki iliyopita watu kadhaa walipoteza maisha kufuatia jengo liloporomoka nchini Sierra Leone