Sinopsis
Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.
Episodios
-
Maaskofu wa kikatoliki nchini Kenya wakosoa utawala, Rwanda yamaliza Marbug
16/11/2024 Duración: 20minMaaskofu wa kanisa katoliki nchini Kenya wameukosoa utawala wa Ruto, wataka kukomeshwa, utekaji nyara na ukiukaji wa haki za binadamu, wapinzani nchini DRC wajitokeza kupinga mpango wa kubadilisha katiba, Rwanda yafanikiwa katika mapambano yake dhidi ya ugoinjwa wa Murbag, kura ya maoni kuhusu katiba mpya kufanyika jumamosi nchini Gabon,Kamati maalum ya Umoja wa Mataifa yaunga mkono ripoti kwamba Israel inatekeleza mauaji ya kimbari jijini Gaza
-
Uchaguzi wa Marekani, mapigano DRC, kampeni za Raila kuwania uenyekiti wa tume ya AU
09/11/2024 Duración: 20minDonald Trump achaguliwa kuwa rais wa 47 wa Marekani, Ziara ya rais wa Kenya William Ruto huko Addis Ababa Ethiopia, na Sudan Kusini, na Raila Odinga kuzindua azma yake ya kuwania uenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika, kuelekea uchaguzi huo utakaofanyika Februari mwaka 2025. Mapigano makali kati ya waasi wa M23 na wazalendo mashariki mwa DRC, Umoja wa Mataifa wasema uamuzi wa kuahirishwa uchaguzi nchini Sudani Kusini haukubaliki, Duma Boko atawazwa rasmi kama rais mpya wa Botswana, Uhusiano wa Urusi na Marekani baada ya Trump kushinda uchaguzi
-
Kithure Kindiki aapishwa kuwa makamu wa rais Kenya, ziara ya rais wa DRC nchini Uganda
02/11/2024 Duración: 20minKuapishwa kwa makamu mpya wa rais wa Kenya Profesa Kithure Kindiki, ziara ya rais wa DRC Félix Tshisekedi Kampala Uganda huku mapigano kati ya waasi wa M23 na wazalendo yakiripotiwa mashariki mwa nchi yake, mkutano wa Comesa watamatika Jijini Bujumbura Burundi, Umoja wa mataifa wasema hali ya kibinadamu nchini Sudan yatia wasiwasi, upinzani washinda uchaguzi mkuu Botswana, kampeni za lala salama Marekani, lakini pia kauli ya Korea Kaskazini kuwa itasimama na Urusi hadi ushindi wake huko Ukraine.
-
Rais Tshisekedi asema katiba ya Congo itarekebishwa, kesi ya naibu rais wa Kenya
26/10/2024 Duración: 20minKauli ya rais wa DRC kuhusu marekebisho ya katiba yazua hisia mseto, kesi ya naibu wa Rais wa Kenya aliyeenguliwa madarakani Rigathi Gachagua yaendelea, umoja wa Ulaya kuendeleza shinikizo ilizoiwekea Burundi mwaka 2015 hadi mwaka 2025. Ziara ya mkuu wa UNHCR Fillipo Grandi nchini Uganda, mgombea wa chama tawala kule Msumbiji awa mshindi wa uchaguzi mkuu, uchaguzi mkuu wa Marekani na mengineyo.
-
Naibu rais wa Kenya Gachagua atimliwa, usalama wa mashariki ya DRC wajadiliwa Luanda
19/10/2024 Duración: 20minKuondolewa madarakani kwa naibu wa rais wa Kenya Rigathi Gachagua na uteuzi wa profesa Kithure Kindiki, serikali ya Kinshasa yakaribisha makubaliano yaliyoafikiwa kati ya mawaziri wa mambo ya nje wa DRC na Rwanda kuhusu suala kulitokomeza kundi la FDLR na Rwanda kusema iko tayari kuwaondoa wanajeshi kwenye ardhi ya Congo, maandamano ya upinzani kule Msumbiji baada ya uchaguzi mkuu, kuuawa kwa kiongozi wa Hamas Yahya Sunwar, uchaguzi mkuu wa Marekani na mengineyo.
-
Mchakato wa kuondolewa madarakani naibu rais wa Kenya, mazishi ya waliokufa Goma
12/10/2024 Duración: 20minWabunge 281 walipiga kura ya ndio kumwondoa naibu wa Rais wa Kenya Rigathi Gachagua madarakani, mazishi ya watu waliokufamaji katika ajali ya Meli huko Goma DRC, ziara ya mkurugenzi wa kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa barani Afrika, Dr Jean Kaseya, nchini Rwanda kutathmini mikakati ya kupambana na mlipuko wa MPOX pamoja na marburg, mafuriko makubwa nchini Mali, mashambulio ya jeshi la Israeli dhidi ya ngome za Hezbollah nchini Lebanon, mchakato wa uchaguzi mkuu kule Marekani. Ungana na Ruben Lukumbuka kusikiliza zaidi
-
Mswada wa kumwondoa naibu rais wa Kenya Kachagua, watu zaidi 78 wafamaji DRC
05/10/2024 Duración: 20minMakala imeangazia mchakato wa kumwondoa madarakani naibu wa rais wa Kenya Rigathi Gachagua, makumi ya watu wafamaji katika ajali ya boti huko Goma mashariki mwa DRC, hali nchini Rwanda na ugonjwa wa murburg, Uganda na Sudan, siasa za Nigeria na maeneo mengine ya Afrika magharibi, mashambulio ya jeshi la Israeli dhidi ya ngome za Hezbollah nchini Lebanon na yale ya Hezbollah nchini Israeli na mambo mengine.
-
Lisu kuishitaki Tanzania kwa jaribio la kumuua, Kenya kupeleka polisi Haiti
28/09/2024 Duración: 20minMwanasiasa wa upinzani kule Tanzania Tundu Lisu kuishitaki serikali na kampuni ya mawasiliano TIGO kwa jaribio la kumuua, rais wa Kenya William Ruto alisema polisi 2500 watapelekwa Haiti, wakati rais wa DRC Félix Tshisekedi atoa wito kwa jumuia ya kimataifa kuiwekea vikwazo Rwanda kwa kuivamia nchi yake na kushirikiana na waasi wa M23, hali nchini Sudan, siasa za Senegal na maeneo mengine ya Afrika magharibi, mashambulio ya jeshi la Israeli dhidi ya ngome za Hezbollah nchini Lebanon na mengineyo.
-
Rais wa Tanzania Samia Suluhu na wanadiplomasia, msamaha kwa mkuu wa polisi Kenya
21/09/2024 Duración: 20minMakala hii imeangazia kauli ya rais wa Tanzania kwa mabalozi wanaowakilisha nchi zao ilivyozua gumzo katika uga wa kimataifa, msamaha wa mahakama kwa afisa mkuu wa polisi Kenya, ziara ya mjumbe wake katibu mkuu wa umoja wa mataifa anayehusika na masuala ya kibinadamu ulinzi wa amani Jean Pierre Lacroix huko DRC, UN kughadhabishwa na kuahirishwa uchaguzi wa sudan Kusini, jeshi Ia Israeli lashambulia Hezbollah kwa kulipua vifaa vyao vya mawasiliano na kwengineko duniani.
-
Uchunguzi wa miili ya wanafunzi waliokufa Kenya, hali ngumu ya wakimbizi DRC na mengineyo
14/09/2024 Duración: 20minNi wiki iliyoshuhudia matukio mengi miongoni ni pamoja na serikali ya Kenya kuendelea na uchunguzi wa mkasa wa moto uliowauwa wanafunzi, maandamano ya maelfu ya wakimbizi kwenye mji wa Goma mashariki mwa DRC wakiomba serikali iwarejeshe makwao na kumaliza vita, kule Senegal rais Bassirou alilivunja Bunge la taifa, na mdahalo wa kwanza wa televisheni kati ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump na makamu wa rais Kamala Harris wanaowania kiti cha urais katika uchaguzi wa Novemba na mengineyo.
-
Mkutano wa 9 China na Afrika, miili200 yazikwa DRC, wanafunzi 17 wateketea Kenya.
07/09/2024 Duración: 20minMakala hii imeangazia mkutano wa tisa kati ya China na Afrika huko Beijing, wafungwa zaidi ya 100 waliuawa katika gereza la makala nchini DRC, Kenya na mkasa wa moto ulivyowaua wanafunzi Kaunti ya Nyeri, uchaguzi kufanyika nchini Tunisia, na nchini Ufaransa Michel Barnier aliteuliwa kuwa waziri Mkuu, miezi miwili baada ya mvutano wa kisiasa nchini Ufaransa, na mambo mengine kwengineko duniani.
-
Kampeni ya Odinga kuwania uenyekiti tume ya AU, DRC yafungua kesi dhidi ya Rwanda
31/08/2024 Duración: 20minUzinduzi wa kampeni ya aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga, anayegombea unyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika, kongamano la 74 la WHO mjini Brazzaville, nchini Congo, DRC na Kampeni inayoitwa ICC Haki kwa DRC, hali ya usalama kuendelea kuzorota nchini Sudan, shambulio la kigaidi Burkina Faso laua zaidi ya watu 300, hali nchini Israeli, na mchakato wa uchaguzi wa Marekani mwezi Novemba
-
DRC yaathirika na M-Pox, Raila asema siasa za Kenya, basi! na mengineyo
24/08/2024 Duración: 20minTumeangazia katika makala ya wiki hii ni pamoja na ugonjwa wa Mpox ulitangazwa kuwa dharura ya kimataifa, DRC ikiathirika zaidi, nchini Kenya Raila Odinga kutojihusisha tena na siasa, jeshi la Uganda lilivamia na kuharibu kambi ya kundi la waasi la LRA huko Sudan pande hasimu zasusia mkutano wa Geneva, nchini Marekani, makamu wa rais Kamala Harris akubali uteuzi wa chama chake cha Democratic kuwa mgombea wa nafasi ya urais, na mengineyo
-
Mpox yatangazwa janga la kimataifa la kiafya, mwanahabari wa Burundi Irangabiye aachiwa na mengineyo
20/08/2024 Duración: 20minMatukio ya dunia yaliyokithiri vichwa vya habari ni pamoja na virusi vya Mpox kutangazwa kuwa janga la dharura la kiafya huku bara la Afrika likiathiriwa zaidi, Burundi yamwachia mwanahabari aliyehukumiwa kifungo cha miaka 10, tutaangazia siasa za Tanzania baada ya wanasiasa wa upinzani kukamatwa baadaye wakaachiwa, lakini pia hatua za mazungumzo kule Geneva kuhusu amani nchini Sudan. Pia tutaangazia mgomo wa vyombo vya habari nchini Senegal kadhalika tutachambua wito wa Umoja wa Mataifa kutaka Afrika kupewa kiti cha kudumu katika baraza la usalama la umoja huoKule Gaza, kundi la Hamas limekataa masharti 'mpya' ya upatanishi na Israeli na mazungumzo ya kupata mkataba wa kusitisha vita hivyo, kurejelewa tena wiki hii jijini Cairo, Misri.
-
Tshisekedi amshutumu mtangulizi wake Kabila, serikali mpya Kenya na mengineyo
10/08/2024 Duración: 20minMakala ya Juma hili imeangazia hukumu iliyotolewa dhidi ya kiongozi wa chama cha waasi wa M23/AFC mashariki mwa DRC Corneille Nangaa, Rais wa Kenya aapisha baraza jipya la mawaziri miongoni mwao wanasiasa wa upinzani, mapigano ya nchini Sudan, maandamano nchini Nigeria na uongozi mpya wa mpito nchini Bangladesh baada ya kutoroka kwa waziri mkuu pia tumengazia yaliyojiri kwengineko duniani.
-
Hamas yalaani mauaji ya kiongozi wake, mauaji ya kimbari DRC Genocost, na mengineyo
03/08/2024 Duración: 20minMakala hii imeangazia kuuawa kwa kiongozi wa kundi la Hamas, Ismail Haniyeh nchini Iran, mazishi yake yalifanyika Doha, Urusi, mataifa ya Magharibi wabadilishana wafungwa, waziri mkuu wa DRC Judith Suminwa aongoza kumbukumbu ya mauaji ya halaiki ya wakongo maarufu, Genocost, yaliyojiri nchini Kenya, na mgomo wa wafanyabiashara wa Uganda, hukumu dhidi ya dikteta wa zamani wa nchini Guinea na kwengineko duniani.
-
Michezo ya olimpiki yaanza Paris Ufaransa, Siasa za Kenya, DRC na kwengineko
27/07/2024 Duración: 20minMakala imeangazia hafla ya ufunguzi wa michezo ya Olimpiki ya Paris siku ya Ijumaa ya wiki hii, huku miundombinu ya treni za umeme ikishambuliwa, rais William Ruto atangaza baraza la mawaziri akiwajumuisha wanasiasa wanne wa upinzani, kesi dhidi ya kiongozi wa muungano wa waasi Corneille Nangaa jijini Kinshasa nchini DRC, Maandamano na kukamatwa kwa vijana kule Uganda, siasa za Afrika Magharibi, na Kaskazini,Joe Biden ajijiondoa katika ki nyang’anyiro cha uchauguzi huku Kamala Harris akiteuliwa kuwa mgombea wa chama cha Demokratic nchini Marekani.
-
Ruto ateua mawaziri wapya, Paul Kagame ashinda uchaguzi, usalama bado mashariki DRC
20/07/2024 Duración: 20minMakala hii imeangazia hatua ya rais wa Kenya William Ruto ya kuwateua mawaziri wapya baada ya mashinikizo, nchi yake ikishuhudia maandamano ya vijana, Kukamatwa kwa mshukiwa wa mauaji ya watu ambao miili yao ilikutwa jalalani Kware jijini Nairobi akiri kuwaua wanawake 42, rais wa Rwanda Paul Kagame ashinda uchaguzi kwa kishindo, Waasi wa M23 na jeshi la congo FARDC wakubali kusimamisha vita baada ya Marekani kutangaza kuongeza muda wa siku 15 kuruhusu misaada ya kibinadamu...na mengineyo..kwengineko duniani ambako watu wamestushwa ulimwenguni kuhusu hitilafu iliyojitokeza kiteknolojia..-
-
Rais Ruto avunja baraza la mawaziri, uchaguzi huko Rwanda, usalama wazorota DRC
13/07/2024 Duración: 20minMakala ya yaliyojiri wiki hii imeangazia hatua ya rais wa Kenya William Ruto kulivunja baraza lake la mawaziri, huku inspekta mkuu wa polisi Japhet Koome akubali kujiuzulu, raia nchini Rwanda wajiandaa kushiriki uchaguzi mkuu wa rais na wabunge nchini Rwanda jumatatu ya julai 15, pia hali ya mapigan yashuhudiwa nchini DRC licha ya wito wa Marekani wa kusitishwa mapigano kwa sababu za kibinadamu.Hali iliyojiri kwenye nchi za Afrika magharibi na kaskazini, Ufaransa, na Marekani.
-
DRC: Wanajeshi wanaodaiwa kutoroka adui kwenye mapambano wahukumiwa
06/07/2024 Duración: 20minMiongoni mwa yale utakayosikia katika makala ya wiki hii ni pamoja na hatua ya Rais wa Kenya William Ruto kuzungumza na wapiga kura kwa njia ya mtandao wa X, wanajeshi waliotoroka adui DRC kuhukumiwa na vilevile mkutano wa nchi za Sahel zinazoongozwa na wanajeshi.