Sinopsis
Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.
Episodios
-
Ukosefu wa maji salama unavyozidisha hali ya kibinadaam barani Afrika
26/03/2025 Duración: 10minKuna idadi kubwa ya watu wanaoshindwa kupata maji salama kwa matumizi ya nyumbani ,hospitali na hata mashamba Uhaba wa maji unaorodheshwa kuwa sababu kubwa ya watu kukosa chakula, kujikimu katika nchi zinazoshuhudia migogoro.Katika nchi kama Sudan na DRC kuna ripoti za hospitali ,kambi za wakimbizi kukosa moja hivyo mashirika ya kimsaada yanapata changamoto kuwahudumia wakimbizi
-
Mpango wa lishe katika shule za umma nchini Kenya kupambana na utapiamlo
19/03/2025 Duración: 10minUkosefu wa lishe bora huathiri afya na elimu nchini Kenya Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la linalowahudumia Watoto (UNICEF) imeonesha kuwa takriban watoto milioni mbili nchini Kenya wanakabiliwa na matatizo yanayotokana na utapiamlo. Mipango ya lishe bora shuleni eneo la Nyanza na maghari mwa Kenya umeonekana kuwa suluhu huku wanafunzi wakipata vyakula vilivyo na virutubishi bora vinavyosaidia kuboresha kinga ya mwili,hivyo kuimarisha afya .
-
Haja ya huduma muhimu za wanawake waja wazito kupatikana kwa urahisi
11/03/2025 Duración: 10minWHO imetaja ukosefu wa huduma za kuokoa maisha wakati wa kujifungua huchangia vifo vingi vya wanawake waja wazito Huduma hizo za wanawake hata hivyo zina bei kubwa
-
Hali halisi ya Malaria barani Afrika wakati huu ufadhili ukiendelea kushuka
10/03/2025 Duración: 10minSerikali za Afrika zitalazimika kuchangia ufadhili wa mipango ya kupambana na Malaria kufidia pengo kubwa la ufadhili Muungano wa viongozi wa Afrika wa kupambana na Malaria ,Africa Leaders Malaria Alliance unasema Afrika inahitaji dola bilioni 5 nukta nane mwaka huu wa kifedha hadi 2026.Hali hii pia imechangiwa na Marekani kukata ufadhili wa misaada kwa nchi za kigeni
-
Kukata kiu ya jamii zinazoishi mpaka wa Kenya na Somalia ,waathiriwa wa mgogoro
25/02/2025 Duración: 08minMamia ya wakaazi wa kaskazini mashariki mwa Kenya maeneo yanayopakana na Somalia na waathiriwa wakubwa wa mzozo wa Somalia hawajakuwa na maji masafi , hali hiyo ikizidisha mgogoro wa kijamii ndani ya jamii hii ya wafugaji wanaotokea upande wa Kenya na upande mwingine wa Somalia. Kukabili hali hii ,kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu , International Committee of the Red cross ,ICRC , shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya ,Kenya Red Cross,KRC katika mkakati wa kuleta amani na ustawi imekuwa ikifanya miradi ya kuwapa wakazi maji .Carol Korir amezuru eneo la Masalani ,kaunti ya Garissa kilomita chache na msitu wa Boni ambapo Al shabab wamekuwa wakifanya mashambulizi na kujificha .
-
Utayari wa ukanda wa Afrika kupambana na magonjwa ya milipuko
19/02/2025 Duración: 10minKatika siku za hivi punde magonjwa ya milipuko imeripotiwa katika mataifa ya Afrika ,ikiwemo Ebola Marburg na Mpox
-
Juhudi za Guinea kumaliza ugonjwa wa Malale mojawapo ya magonjwa yaliyotengwa
05/02/2025 Duración: 10minGuinea itakuwa ni taifa la nane la Afrika kuthibitishwa kuangamiza ugonjwa wa malale Guinea imekuwa ilishiriki katika majaribio ya matibabu ya ugonjwa wa malale ambayo yalifanyiwa utafiti mara ya kwanza nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya CongoTimu ya madaktari kutoka DRC na Guinea walishirikishwa kwenye majaribio hayo na kwenye makala haya tumezungumza na Dkt Chirac Bulanga kutoka DRC
-
Ugonjwa wa Ukoma bado ni changamoto kubwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
29/01/2025 Duración: 09minDRC imeripoti maambukizi ya Ukoma mwisho wa mwaka jana na pia mwaka huu Ukoma ni ugonjwa unaoathiri sana ngozi na unaweza kuharibu baadhi ya viungo kama vile mikono ,miguu na hufanya mtu kutengwa na jamii
-
Ongezeko la mafua na magonjwa yenye dalili za mafua wakati wa joto
21/01/2025 Duración: 09minKumeendelea kushuhudiwa kwa idadi kubwa ya watu wanaougua mafua au magonjwa yanayoathiri mfumu wa kupumua mwezi Januari ambao una joto jingi na vumbi. Hii inajiri wakati China ikiwa imeripoti mlipuko wa ugonjwa wa Human metapneumovirus ,HPMV unaofanana na COVID 19 .Daktari Juma Maleve kutoka Hospitali ya rufaa ya Mombasa ,Pwani ya Kenya anafafanua.
-
Dunia: Zaidi ya watu Milioni 18 wameathirika na ugonjwa wa mtindio wa ubongo
07/01/2025 Duración: 10minKwa kitaalam mtindio wa ubongo unaitwa Cerebral Palsy kwa kifupi CP..ugonjwa huu unatokana na jereha kwenye ubongo ambao huwa linafanya mtoto kushindwa kudhibiti misuli ya mwili wake hali inayoweza kusababisha viungo vya mtoto kulegea au kukamaa muda wote. Mtoto anaweza kupata majeraha kwenye ubongo akiwa bado yuko tumboni, wakati wa kuzaliwa au baadae maishani.CP husababisha ulemavu wa kudumu katika maisha yote ya mtoto.
-
Uzazi wa Mpango:Wanaume wajitolea kufanya upasuaji wa mirija -Vasektomia
31/12/2024 Duración: 09minVasectomy ni njia ya kupanga uzazi ambayo inahusisha upasuaji wa mshipa unaopitisha mbegu za kiume, ili mme asiweze kumpachika mke mimba. Ni njia ya upangaji uzazi ya milele.Na pengine unajiuliza hili linafanyiikaje na ina athari gani kwenyen afya ya mwanaume ?Sikiliza makala haya
-
Kupanga uzazi kwa kutumia njia za homoni na ile ya Kitanzi -Matatizo ya Afya kwa Wanawake
24/12/2024 Duración: 10minKwenye awamu yetu ya Kwanza tuliangazia njia za asilia walizokuwa wanatumia nyanya zetu kabla ya sayansi kuingia.Tukataja njia ya Kalenda,mipira ya kondomu na kumwaga mbegu za kiume nje ya njia ya uzazi almaarufu Withdrawal.Hivyo basi kwenye sehemu hii ya pili tutaangazia njia za homoni na zisizo za homoni na ambazo asilimia kubwa ya wanawake wanatumia.Kama vile vidonge, vipandikizi ,sindano, na IUD.
-
Uzazi wa mpango kwa njia asilia
17/12/2024 Duración: 09minMakala haya yanaangazia upangaji kupanga uzazi, na jinsi linavyohusiana na afya ya mwanamke. Kupanga uzazi ni sehemu muhimu ya afya, kwani husaidia wanawake kudhibiti idadi ya watoto wanapokuwa nayo, na pia ina athari kubwa katika afya yao ya kimwili na kihisia.
-
Juhudi za kupunguza matumizi ya dawa za kulevya eneo la Pwani ya Kenya
13/12/2024 Duración: 10minIdadi ya vijana wanaotumia dawa za kulevya katika umri mdogo imeongezeka
-
Maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani
09/12/2024 Duración: 09minKatika makala haya, tutazungumza na watu muhimu kama vile mgonjwa wa UKIMWI, daktari, na mkunga anayeelimisha kuhusu jinsi ya kuzuia watoto kuambukizwa virusi vya UKIMWI wakati wanapozaliwa. Pamoja, tutafahamu changamoto, mafanikio na hatua zinazochukuliwa katika vita hivi.
-
Dunia: Wahudumu wa afya waendelea kuuawa katika maeneo ya mizozo
07/12/2024 Duración: 10minUmoja wa mataifa umeorodhesha mwaka 2024 kama mwaka hatari zaidi kwa wafanyikazi wa mashirika ya kimsaada Katika takwimu za UN ,wafanyakazi zaidi ya 200 wamewauwa katika mzoz wa Gaza na wengine zaidi ya 20 katika mzozo wa Sudan
-
Afya ya kujifungua na uzazi: Changamoto zinazotokea wakati wa kujifungua mtoto
12/11/2024 Duración: 10minIdadi kubwa ya kina dada wameamua kuchagua upasuaji kama njia rahisi ya kujifungua kwa sababu tofauti tofauti.Sehemu ya pili ya makala haya inaangazia ni kwa nini idadi hio inaongezeka kisha hali inakuaje pale kwenye chumba cha kujifungulia.Dakatari Lilian Nkirote kutokea hospitali ya Jacaranda jiji Nairobi anaelezea kwa kina.
-
Afya ya uzazi na kujifungua
08/11/2024 Duración: 10minMakala ya siha njema wiki hii tunaangazia Afya ya uzazi na kujifungua na sio safari nyepesi.Ni safari yenye changamoto haba na furaha kwa wanawake na familia zao. Ni muhimu kwa kila mama mjamzito kufahamu hatua muhimu za kuhakikisha ustawi wa afya yake na ya mtoto anayemtarajia. Kupitia huduma bora za kiafya na ushauri wa wataalamu, wanawake wanaweza kufurahia safari ya uzazi kwa usalama na utulivu.
-
Juhudi za kikanda kukabiliana na tatizo la kiafya la kungatwa na nyoka
29/10/2024 Duración: 08minKumekuwa na mikakati maksudi katika nchi za Afrika kuwekeza katika utafiti kuhusu nyoka na matibabu ya simu yake Baadhi ya mikakati hiyo ni utafiti wa kuwa na aina moja ya dawa ambayo inaweza kutumika katika nchi za Afrika Mashariki vile vile kuelimisha jamii kuhusu huduma za kwanza sahihi kuwasaidia wagonjwa na namna ya kuzuia madhara zaidi kutokana na sumu ya nyoka.
-
Kukabiliana na tatizo la kiafya la kungatwa na nyoka katika ukanda wa Afrika
22/10/2024 Duración: 10minKungatwa na nyoka imeorodheshwa miongoni mwa matatizo ya kiafya yaliyotengwa Takwimu za shirika la afya duniani ,WHO zinasema kila dakika nne ,watu nne duniani, hupoteza maisha kutokana na sumu ya nyoka.Hii ni kutokana na gharama ya juu ya matibabu ,ugumu wa kupatikana na matibabu haya na raia kutofahamu hatua sahihi ya kufuata ukiumwa au kutemewa sumu na nyoka.Nchini Sudan Kusini ,visa vya wagonjwa wanaongatwa imeongezeka maradufu kutokana na mafuriko ya miezi kadhaa kwa mujibu wa shirika la madaktari wasio na mipaka,MSFMSF hata hivyo kudhibiti hali ,inatumia mfumo wa akili mnemba au AI kurahisisha ubainishaji wa ainya ya nyoka na sumu yake vile vile matibabu yake,mradi unaoendeshwa na MSF katika baadhi ya vituo vyake jimbo la Warrap na Abyei.