Sinopsis
Kwenye makala ya Afrika ya Mashariki unahabarika na kuelimika juu ya changamoto za maisha ya wananchi wa Afrika Mashariki na eneo zima la maziwa makuu. Usipitwe na Makala ya Afrika ya Mashariki kwani unapata nafasi ya kutoa mawazo yako na kusikiliza wataalamu mbalimbali watakaokuwezesha kubadili fikra na kufikia maendeleo endelevu.
Episodios
-
Changamoto za raia wa Afrika Mashariki kupata maji kwa ukaribu
28/06/2024 Duración: 09minMakala ya Afrika mashariki ikiangazia juu ya namna wakazi wa Jumuiya ya Afrika mashariki wakiwa katika mkwamo wakupata katika huduma ya maji kwa ukaribu licha uwepo wa vyanzo vikumbwa vya maji. Kwa mujibu wa tovuti ya Jumuiya ya Afrika mashariki, Maziwa makubwa yote mawili kwa maana ya ziwa Victoria na Tanganyika, na hatimaye, Mto White Nile hutegemea vyanzo vya maji vya kikanda vinavyojulikana kama Minara ya maji Water Towers ya eneo hilo.Minara ya Maji ya Afrika mashariki ni mkusanyiko wa mazingira ya milimani na mabonde ya mito yanayohusiana.Maeneo haya yana ushawishi mkubwa kwa hidrolojia ya kikanda na mizunguko ya hali ya hewa duniani.Licha ya uwepo wa minara hii bado serikali za wanachama wa jumuiya hii zipo katika mkwamo wakufikisha huduma za maji kwa wananchi walio wengi.
-
Tanzania: Kufungwa kwa muda kwa uvuvi ndani ya Ziwa Victoria
22/06/2024 Duración: 09minSerikali inasema hatua hiyo ya kufungwa kwa giza inalenga kuwapa nafasi samaki wadogo kua.
-
Mvutano kati ya Somalia na Ethiopia kuhusiana na suala la Somaliland
08/06/2024 Duración: 09minKatika Makala ya Afrika mashariki hii leo tunatuwa pembe ya Afrika tukiangaza juu ya vuta nikuvute katika serikali ya mjini Mogadishu na Addis Ababa.