Gurudumu La Uchumi

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 3:58:19
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika. Mada hizi zinafanyiwa utafiti wa kina na zinazungumzwa kwa lugha rahisi inayoeleweka ili kukufanya uelewe na usichoke kusikiliza .

Episodios

  • Athari za utoroshaji na utakatishaji fedha barani Afrika

    02/10/2024 Duración: 09min

    Tatizo la fedha haramu barani Afrika linaligharibu bara hili kiasi cha dola za Marekani bilioni 50 na bilioni 80 kila mwaka, Asilimia 44 ya utajiri wa kifedha wa Afrika inadhaniwa kuwa nje ya nchi. Kwa mujibu wa Ripoti ya Maendeleo ya Uwazi wa Ushuru barani Afrika ya 2023, nchi za Afrika zimeokoa dola bilioni 2 kwa mwaka kutokana na watu kuweka wazi mapato yao, ubora wa kubadilishana taarifa na uchunguzi wa nje ya nchi.Tumezungumza na Ali Mkimo, mtaalamu na mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.

  • Fursa na changamoto ya huduma jumuishi za mifumo ya kifedha kidijitali barani Afrika

    18/09/2024 Duración: 09min

    Msikilizaji kwa mujibu wa benki ya dunia, ni asilimia 49 tu ya watu wazima wanamiliki akaunti benki, takwimu za hivi karibuni zikionesha ongezeko la asilimia 55 mwaka 2021 kutoka asilimia 43 mwaka 2017, hata hivyo kiwango hiki kikiwa kidogo ukilinganisha na wastani wa kidunia wa asilimia 76. Makala ya Gurudumu la Uchumi, juma hili tunajadili kuhusu huduma jumuishi za mifumo ya kifedha barani Afrika. Machambuzi wa masuala ya uchumi ALI MKIMO anajibu maswali kadhaa kuhusu sekta hii.

  • Afrika na usalama wa chakula

    11/09/2024 Duración: 09min

    Msikilizaji juma lililopita Rwanda ilikuwa mwenyeji wa kongamano la mfumo wa chakula barani Afrika, ambapo wadau zaidi ya elfu 4 kutoka kila pembe ya mataifa ya Afrika walishiriki.Mkutano uliangazia kuhusu mifumo ya chakula, mbinu bora na teknolojia  ambazo zinaweza kubadilisha mifumo ya kilimo na chakula barani Afrika na wakati huohuo kutengeneza nafasi za kazi na fursa kwa wanawake.Msikilizaji wiki hii nimeshirikiana na mwanahabari wetu wa Kigali, Christopher Karenzi;

  • Ndio au hapana, mkutano kati ya Uchina na Afrika

    04/09/2024 Duración: 09min

    Uchina wiki hii imekuwa mwenyeji wa mkutano kati yake na viongozi wa Afrika, kwa mujibu wa takwimu zilizoko, China ni taifa la pili duniani kufanya biashara nyingi zaidi na bara la Afrika, biashara inayokadiriwa kufikia dola za Marekani bilioni 167 kwa mwaka. Kuangazia mkutano huu na wasiwasi ulioko kuhusu uwekezaji wa China barani Afrika, tumezungumza na Ali Mkimo, mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara akiwa Tanzania.

página 2 de 2