Sinopsis
Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali.
Episodios
-
Fahamu mchezo wa Tong IL Moo Do kuelekea mashindano ya Mombasa Open 2024
30/11/2024 Duración: 23minTuliyokuandalia ni pamoja na mahojiano ya moja kwa moja na washikadau wa mchezo wa Tong IL Moo Do ambao walitutembelea studioni. Mchezo huu unazidi kukua Afrika. Je, unachezwaje, nini umuhimu wake, umepiga hatua kiasi gani, maandalizi ya makala ya Mombasa Open ya mwaka huu yakoje? Pia tumeangazia Ligi ya Klabu bingwa Afrika, msimu mpya wa raga ya HSBC duniani na Kombe la Mataifa ya Afrika ya kina dada mchezo wa handboli ambayo ilianza wiki hii pamoja na uchambuzi wa mechi za klabu bingwa Ulaya
-
CAF: Droo ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kina dada yakamilika
23/11/2024 Duración: 23minTuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa droo ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kina dada 2024, fainali ya klabu bingwa Afrika kwa kina dada, nini maana ya Tanzania na Uganda kuwakilisha CECAFA kwenye AFCON 2024, mechi za kufuzu ligi ya Afrika ya Basketboli na michuano ya kufuzu Mashindano ya Afrika ya Basketboli, ligi za ukanda na ulaya Pep Guardiola atia saini mkataba mpya klabuni Man City.
-
AFCON 2025: Uganda yafuzu fainali za mwaka kesho huku Kenya, Ghana zikitupwa nje
16/11/2024 Duración: 23minTuliyoyazungumzia ni pamoja na upekee wa klabu ya voliboli nchini Kenya ya Trailblazers, uchaguzi wa FKF nchini Kenya umeanza, mabadiliko ya makocha klabuni Yanga, timu ya taifa ya Kenya ya walemavu ya soka yamaliza nafasi ya nne Kombe la Dunia, uchambuzi wa michuano ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2025 na pigano la Jake Paul dhidi ya Mike Tyson
-
CAF: Ligi ya klabu bingwa barani Afrika 2024 kwa kina dada yaanza nchini Morocco
09/11/2024 Duración: 23minTumeangazia klabu ya Chaux Sport kutoka DRC kubanduliwa kwenye mechi za kufuzu Ligi ya Basketboli Afrika 2024, masaibu ya Yanga SC nchini Tanzania, uchaguzi wa FKF nchini Kenya, mashindano ya kuendesha baiskeli Afrika kwa kina dada nchini Burundi, kifo cha rais wa soka nchini Algeria, matokeo na uchambuzi wa mechi za klabu bingwa Ulaya na fainali ya tenisi kwenye mashindano ya WTA