Sinopsis
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa
Episodios
-
Rwanda na DRC zawasilisha mapendekezo kuhusu mkataba wa amani
07/05/2025 Duración: 10minRwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zimewasilisha mapendekezo ya rasimu ya mkataba wa amani kwa Marekani, kujaribu kutafuta mzozo wa Mashariki mwa DRC. Nchi hizo mbili zinatarajiwa kutia saini mkataba wa kudumu mwezi Juni, jijini Washington. Harakati hizi, zitazaa matunda ?
-
Kenya: Upinzani utamtikisa Ruto uchaguzi wa mwaka 2027 ?
30/04/2025 Duración: 10minWanasiasa wakuu wa upinzani nchini Kenya, wakiongozwa na aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua, Aprili 29 2025, walikutana jijini Nairobi kuanza mikakati ya kuunda muungano mpya, kwa maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Je, muungano huu ambao pia umemjumuisha aliyekuwa Waziri wa usalama Fred Matiang’i, unaweza kumtikisa rais William Ruto wakati wa uchaguzi huo ?
-
DRC: Kabila aripotiwa kufikia Goma, huku chama chake kikifungiwa
23/04/2025 Duración: 10minRais wa zamani wa DRC, Joseph Kabila, Aprili 18, aliripotiwa kurejea nchini na kufikia jijini Goma, linalodhibitiwa na waasi wa M 23. Hata hivyo, taarifa hizi hazijathibitishwa rasmi. Serikali jijini Kinshasa, nayo imesitisha shughuli zote za kisiasa za chama chake cha PPRD. Kabila anashtumiwa na serikali kwa kuunga vitendo vya waasi hao.
-
Tundu Lisssu afunguliwa kesi ya uhaini, CHADEMA matatani
16/04/2025 Duración: 09minMwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA, Tundu Lissu, Aprili 10 alifunguliwa kesi ya uhaini, baada ya kukamatwa akiwa kwenye kampeni ya kisiasa, kushinikiza mageuzi kwenye mchakato wa uchaguzi, uliopangwa kufanyika mwezi Oktoba.