Habari Za Un
Mafunzo ya walinda amani kutoka Tanzania huko Beni yajengea uwezo walimu kusaidiana na watoto
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editor: Podcast
- Duración: 0:02:25
- Mas informaciones
Informações:
Sinopsis
Umoja wa Mataifa unasema kwamba vita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC imefanya taifa hilo kuwa pahala hatari zaidi duniani kwa watoto kuishi, kutokana na mateso ya kimwili na kisaikolojia wanayoyapitia. Kwa kutambua hilo walinda amani wanawake wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanaohudumu kwenye ujumbe wa UN nchini humo, MONUSCO wamechukua hatua kuona watoto wanaishi kama watoto. Video ya MONUSCO ikianza na walinda amani wakijongea kwa jamii, Kapteni Noella Nyaisanga kiongozi wa kikundi hicho cha wanawake cha kikosi cha 11 cha walinda amani wa Tanzania kwenye MONUSCO, TANZBATT-11 anaeleza jinsi kikundi chao kinavyosogea kwa jamii na hasa watoto ili kutatua changamoto zinazowakabili kutokana na mapigano kati ya jeshi la serikali na waasi kwenye eneo hili la Beni, jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa DRC. Anafafanua zaidi lengo lao.Lengo ni kujenga uaminifu kwa raia ambao tunawalinda. Kwa hiyo tukaamua kuandaa masomo shuleni, ambayo yataweza kuwaimarisha wao, kuwasaidia tatizo la kuwa